Wapenda Michezo Tutamkumbuka Jakaya

Wapenda Michezo Tutamkumbuka Jakaya

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Kwa tuliofuatilia sherehe za kumuaga rais anaemaliza muda wake mh Jk jana ktk sherehe zilizoandaliwa na Taswa mtakubaliana nami kua rais wetu huyu amekua tofauti sana na waliomtangulia ktk kupiga jeki gurudumu la maendeleo ktk sekta ya michezo,

ki ukweli amejitaahidi kwa uwezo wake wote alioweza kuinyanyua tasnia hii ,pamoja na mengi alioongea ktk hotuba yake na mtazamo wake katika swala zima la michezo,kusaidia ktk uanzishwaji wa kituo kipya cha michezo kwa watoto cha kidongo chekundu kitakachozinduliwa wiki hii jumamosi,

shime viongozi wa michezo shikeni na mfanyie kazi mawazo na ushauri wake rais,Jakaya Kikwete hakika wewe ni mwanamichezo wa kweli sisi tutaendelea kuhitaji msaada wako pale utapoona inafaa kushauri kiukweli tutakukumbuka Kikwete sie wapenda michezo,twasema ahsante kwa yote.
 
Tutolee hapa... ainisha nini kimebadilika kwenye michezo tangu kaingia huyo unaemsifia
 
Michezoo na wasanii, wameenjoy sana. Vp wanasayansi wetu, walimu na watumishi wengine toeni ushuhuda na nyinyi
 
Huwezi kuutambua umuhimu wa mtu akiwa yupo lakn mapaka atakapoondoka ndio utaujua umuhimu wake.
Tukae tusubir
 
Atakumbukwa kwa lipi hasa? Kuna kombe lolote tulichukua katika soka, netiboli nk? Riadha? Tumkumbuke kwa lipi sasa? Tuache unafiki jamani. Hana alilofanya katika michezo huyu - labda Big Brother.
 
Angalau Ben Mkapa tunamkumbuka kwa uwanja. Nilitegemea naye Kikwete atuachie uwanja wenye hadhi katika moja ya miji hii: Mwanza, Arusha au Mbeya.
 
Duu..tuna tofautiana sana ..kawaida mtu atakumbukwa walau kwa kuweka misingi rafik ambayo anaweza yeye au anaemfuta kuendeleza...au kwa kuwezesha timu kuchukua makombe au medali..sasa Jk katka hayo kafanya lipi kwa miaka kumi aliokaa ikulu..nachokumbuka ni katka kipind hiki..tuliletewa kocha wakat tatizo letu sio kocha..wasanii wa muziki wakapewa studio wakat tatizo lao sio studio...hizo ni siasa za watu wanajikomba
 
mkapa ndio wakukumbukwa, zawadi ya uwanja mpya wa taifa ni zawadi bora kuliko hizo za kikwete
 
Back
Top Bottom