Wapendwa katika yeye tuanze na hii kuhusu ndoa na mahusiano

Wapendwa katika yeye tuanze na hii kuhusu ndoa na mahusiano

GoLC

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2025
Posts
268
Reaction score
466
Hodi humu mabibi na mabwana.

Kwa heshima na taadhima naomba mnialike humu rasmi kwa maana humu ndimo kutakuwa makao yangu kwa asilimia nyingi. Nina ujumbe mzuri na mwingi kuhusu ndoa na mahusiano. Hata hao kataa ndoa wako na mtizamo huo kwa kuwa pengine hawakuwa na mtizamo sahihi kuhusiana na ndoa na mahusiano.

Kwa leo tutanza na hoja hii fupi ila nzito; kwamba “Mungu aliumba mwanamke kutoka kwa ubavu wa mwanaume ili awe karibu na moyo wake, si chini ya mguu wake.”

Tuanzie hapo. Mwanaume akitambua hilo, unyanyasaji hautakuwepo. Mwanamke pia akitambua kuwa kusudio lilikuwa ni hilo, basi anayo nafasi ya kumkumbusha mume wake kuwa kusudi ni hilo na sio lile. Muwe na siku njema sana.
 
🔸 “Ndoa nyingi huzama si kwa upanga, bali kwa neno lisilodhibitiwa. Kila kauli ni mbegu; ukisema, ‘Siku ukifanya hivi, ni mwisho wetu’, jiandae kwa mavuno yake.” 🌾
 
Wakina Delila si mnaitwa huku maana na nyie ni wanyanyasaji wa wanaume mnajificha...
 
Mkuu achana na ayo mambo,baadae njoo apa kitambaa cheupe
Nasikia ziko nyingi. Ila hata kama nikija ni mwendo wa kusambaza neno tu. Wengi hukesha maeneo hayo kwa kuhofia kurudi kwa wenza wao
 
Back
Top Bottom