Wapendwa naona kama mwisho wangu umekaribia

Status
Not open for further replies.
Pole sana mkuu kwa changamoto yako, kaza moyo utavuka. Kama umeoa na wife anaendelea kukuheshimu ni jambo jema. Niliwahi kuanguka pia, tena vibaya sana. Kibaya zaidi hata mke wangu hakuniheshimu hadi aliondoka tena kwa influence ya wazazi wake.

Ila nashukuru nilirudi kwenye njia baada ya kupata kazi yenye mkataba mzuri sana Bwawa la umeme Rufiji. Kuanzia hapo, mambo yakawa poa, nikamaliza mkataba na kuanza kupata deals na kampuni tofauti hadi za mbali na nyumbani. Kwa hiyo amini na uendelee kupambana mkuu. Utashinda
 
Pole mkuu kila mtu ana ups and downs
zake wengine wakikusimulia zao utaona afadhali ya changamoto yako.
 
Huko mbali Sana pia sio suluhisho la changamoto ninazopitia
Dogo tuliiiaa, mke keshaondoka una wasiwasi gani tena. Bila mke unatoboa kirahisi sana.
Pepo limeshakimbia, utalala bila masimango, ukipata hela kidogo huna hofu utamwambia nini kausha damu, sasa una amani sana hata kama huna hela.
Kuna wanawake ibilisi sasa kaenda kujiuza na hela hatapata.
 
Wanawake ibilisi kabisa, huna hela anakuona tàkataka tuu.
 
Pole kwa changamoto unazopitia..
Njia ya kuelekea kwenye mafanikio huwa sio rahisi na wengi huwa wanaamua kukatisha safari na kubaki maskini na wachache wanaovumilia na kuendelea na mapambano hatimae hufika nchi ya ahadi.

Naamini hata aliyekua kakuajiri alikumbana na changamoto hizo mpaka alipofikia hapo.
 
Umefurahi bila kuzingatia kuondoka kwa huyu mke kuna impact gani na gani kwa mtoto wao
Kwani aliyeondoka hakujua kuna impact gani kwa mtoto? Baba anajua kuna impact gani ndo maana kabaki kupambania mtoto.
Sasa kwanini nisifurahi hilo ibilisi lisilojua impact kwa mtoto limeondoka? Angeweza hata kumpa sumu mwanaume ili apate uhuru kufanya umalaya. Sasa kaondoka mumewe ana amani moyoni.
 
Inasikitisha sana

Pole sana na usichoke kupambana kaka

Kuna ukweli mchungu ambao wengi hawaujui na huenda wengine wakaleta kebehi juu yake. Riba, kamari na pombe ni vitu vitatu ambavyo vinamaliza sana uchumi wa watu. Kama mali ya mtu imechanganyika na vitu hivyo au na kingine chochote ambacho kina be termed as haramu kwenye sheria za dini (mfano dhuluma, wizi, ushirikina, zinaa nk) basi mali hiyo ni rahisi sana "kurudi kwao" siku za mbeleni.

Kwa maana hiyo mara nyingine kufilisika inakuwa ni bora kwetu kwani kunatufanya tujue ni wapi tulikosea na tuanze upya kwa njia za halali zaidi
 
Pole sana ndugu, maisha yana ups and down kama ulivyoweza kutoka chini na ukafika kwenyw mafanikio amini nafasi bado unayo tena..
Usikate tamaa angalia fursa kutokana na mazingira yanayokuzunguka fanya kitu ambacho kitakupunguzia mawazo, kwa mfano ingia site fanya kama walivyosema wakubwa hapo kutembeza matunda itakuongezea circle mpya na kuamini vocha iliyokwanguliwa inaweza ikauzwa tena..
Kutembea kwako kunaweza kukupa fursa na bahati ya kupata kazi ambayo hukudhania kabisa
 

Pole kwa changamoto, hilo wazo la kufika mwisho na kukata tamaa liondoe kabisa kwenye kichwa chako.
Sijui wewe ni mtu wa Kaskazini ipi, ila mimi nimeoa huko kwa wachaga, hawa mabwashee zangu sijawahi kusikia wakiongea neno linaloashiria kukata tamaa. Sio kwa wanawake wala wanaume.

Pambana, utasimama tena. Pia kama unaamini katika Mungu, omba sana, kwa simulizi yako matatizo yako yote ni kama yanatokana na mambo ya kishirikina.
 
Mwamba Mungu akusimamie sana na usikate tamaa hao wanaokutazama wana kuhitaji sana mkuu. Endelea kuomba kazi na kujitafuta jipe subira na uvumilivu na kuwa na utulivu fikiria namna ya kujinyanyua tena na tena pia umesomea fani nzuri kibaha kuna viwanda vingi kama wana hutaji mtu wa machenical engering kaombe kwenye vuwanda pia kwa watengeneza barabara nk popote ambapo fani yako ina apply ingia kujaribu one day utacheka tena
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…