Wapenzi wa CHADEMA ndio kundi la watu wenye hasira sana kwa sasa

Dam55

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2015
Posts
5,669
Reaction score
12,044
Wafuasi na wapenzi wa CHADEMA. Kwa maoni yangu binafsi kwasasa hapa nchini wafuasi na wapenzi wa CHADEMA ndio kundi la watu wenye Hasira kali zaidi.

Watu hawa wamegawanyika sehemu mbili

1: Tabaka la Uongozi wa CHADEMA. Viongozi wa hiki chama ni watu wenye Hasira kali Sana, Chuki, husuda, visasi

Ukisikiliza hotuba zao utagundua hilo. Ni watu wenye kutamka maneno makali yenye kubeba hisia nzito kutoka mioyoni mwao ambazo wanatamani watanzania wote wawe nazo. Vyama pinzani vyote vingine wanataka viunge mkono CHADEMA kwa chochote kile watacho sema kinyume na hapo basi ni mamluki wa CCM.

Ikitokea siku moja Tanzania kila mtaa unawaka moto, huku watoto wakibakwa kikatili, kuuawa na vilio kila Kona basi siku hiyo kwao itakuwa ni sherehe kubwa sana.

2: Wafuasi na chama, wapenzi na wakeleketwa. Hawa nao ni watu wenye Hasira kali sana, ni watu wenye maneno makali yenye lengo la kuudhi hata pasipo sababu kabisa.

Mfano Mzuri ni hapa jukwaani ole wako ukianzisha mada isiyo sifu CHADEMA tena bahati mbaya iwe na hoja ngumu kujibika zenye ukweli kuhusu chama chao, hapo ndipo hasira huwaka zaidi. Utakutana na kauli za ajabu Kama:

Mataga
Uza ubongo mana unakaa nao kwa hasara.
Lissu amewasika kunako
Huna akili
Pumba n.k

Wakiambiwa na viongozi wao kuhusu kuandamana kudai haki basi hapo hulipuka kwa shangwe kubwa sana wengine hudiliki kusema damu imwagike!

Muda huo wanakuwa wamesahau kuwa.

Yawezekana mumewe au mke ni wa chama kingine tofauti na yeye.

Mwanaye, mjomba, shangazi, boss wake ofisini, jirani yake, mpangaji mwenzake, mfanya biashara mwenzake, rafiki wa familia yake n.k ni watu wa vyama tofauti na yeye. Hajui kwamba akianza kumwaga hiyo damu itaanzia nyumbani kwake kumwagika.

Kwa kifupi hao ndio CHADEMA a.k.a watanzania wanao ishi kwa hofu kubwa sana kwa mujibu wa maneno yao ya mitandaoni.

Kwa mtu asiye ijua Tanzania au anaye ishi nje ya Tanzania akifuatilia kundi hili la CHADEMA wa mitandaoni anaweza kudhani nchi inawake moto.

Ukitaka kundi hili liwe na furaha sana na uitwe mwenye akili kubwa basi unatakiwa useme:

CHADEMA ndio chama bora Cha siasa kuliko vyote barani Afrika.
Lissu ndio mwanasheria bora zaidi kuliko wote Tanzania.
Lissu ndio binadamu pekee mwenye akili nyingi kuwazidi watanzania wote.

Yote tisa kumi, tukana serikali kwa kadiri uwezavyo hapo utakuwa umewakonga nyoyo zao haswaa.
 
Acha kupotosha mkuu.

1 sijajua kiongozi gani wa CHADEMA mwenye hizo chuki visasi na jasira acha kupotosha. Voongozi wengi pamoja na kujeruhiwana utawala huu wa jiwe kufungwa kufilosiwa kubambikiziwa kesi kutekwa nk bado wameendelea kuwa imara kuongoza jahazi.

2 Ni kweli kabisa mmekuwa mkijibiwa vibaya hapa kwa sababu mlitumwa Na Dk bashiru muje mtujibu bila ya kufikiria. Mmekuwa mkileta nyuziza kijinga sana hapa Nyuzi za kimatanga zile nyuzi za Buku saba nk.

Watanzania tumekuwa tukiishi kwa hofu kubwa sana Jaribu kuvaa viatu vya wazazi wa Mo Anzory Gwanda, Ben saa nane, lissu ,Roma mkatoliki akwilina nk.

Nchi imejaa ubabe mwingi sana na udikteta.
Kuminya uhuru wa vyombo vya habari
Kutekana .
Kumwaga mvua za risasi.
Kuzuia mikutano ya kisiasa 5 years.
Kupoteza watu.
Miili ya watu kuokotwa kwenye viroba nk.
Mauaji ya kibiti nk.

Sijawahi kuona vurugu zozote zikianzishwa na CHADEMA bali Police ndio wamekuwa wakimimina Risasi hadj za moto minyume kabisa na sheria. Mfano maandamano yaliyopelekea Polisi Kumuua Akwilina mwa lengo la kumpiga mbowe risasi nk.

Lissu ni Mwanasheria bora kabisa kuwahi kuzaliwa kwenye hii nchi ameshinda kesi nyingi sana , Amefanya kazi na Taasisi kubwa sana Zenye levo ya kidunia nk nk.

Pia Lissu ndio binadamu pekee aliyepigwa Lisasi 32 akatoka salama.

Mbowe pamoja na kuvunjwa kufilisiwa kudhurumiwa mashamba Bill, Tanzania Daima nk nk
Bado ameendelea kuwa imara kuwapigania watanzania

Usijisahaulishe.
Ni yeye
 
Kuanzia kwa watu wasiojulikana, kupotea Ben Saanane, Azory Gwanda, Mbowe kuharibiwa mali zake, Wakurugenzi na Tume kukata wagombea wao bila sababu za msingi, halafu wewe unakuja kuandika pumba zako.

Ndio ni pumba japo najua hutaki kuliona hilo neno, kama unaona hayo yote wanayofanyiwa Chadema ni mazuri halafu wawe wanatabasamu basi watakuwa mazuzu kama mleta mada.
 
Wafuasi na wapenzi wa CHADEMA. Kwa maoni yangu binafsi kwasasa hapa nchini wafuasi na wapenzi wa CHADEMA ndio kundi la watu wenye Hasira kali zaidi.

Watu hawa wamegawanyika sehemu mbili

1: Tabaka la Uongozi wa CHADEMA. Viongozi wa hiki chama ni watu wenye Hasira kali Sana, Chuki, husuda, visasi

Ukisikiliza hotuba zao utagundua hilo. Ni watu wenye kutamka maneno makali yenye kubeba hisia nzito kutoka mioyoni mwao ambazo wanatamani watanzania wote wawe nazo. Vyama pinzani vyote vingine wanataka viunge mkono CHADEMA kwa chochote kile watacho sema kinyume na hapo basi ni mamluki wa CCM.

Ikitokea siku moja Tanzania kila mtaa unawaka moto, huku watoto wakibakwa kikatili, kuuawa na vilio kila Kona basi siku hiyo kwao itakuwa ni sherehe kubwa sana.

2: Wafuasi na chama, wapenzi na wakeleketwa. Hawa nao ni watu wenye Hasira kali sana, ni watu wenye maneno makali yenye lengo la kuudhi hata pasipo sababu kabisa.

Mfano Mzuri ni hapa jukwaani ole wako ukianzisha mada isiyo sifu CHADEMA tena bahati mbaya iwe na hoja ngumu kujibika zenye ukweli kuhusu chama chao, hapo ndipo hasira huwaka zaidi. Utakutana na kauli za ajabu Kama:

Mataga
Uza ubongo mana unakaa nao kwa hasara.
Lissu amewasika kunako
Huna akili
Pumba n.k

Wakiambiwa na viongozi wao kuhusu kuandamana kudai haki basi hapo hulipuka kwa shangwe kubwa sana wengine hudiliki kusema damu imwagike!

Muda huo wanakuwa wamesahau kuwa.

Yawezekana mumewe au mke ni wa chama kingine tofauti na yeye.

Mwanaye, mjomba, shangazi, boss wake ofisini, jirani yake, mpangaji mwenzake, mfanya biashara mwenzake, rafiki wa familia yake n.k ni watu wa vyama tofauti na yeye. Hajui kwamba akianza kumwaga hiyo damu itaanzia nyumbani kwake kumwagika.

Kwa kifupi hao ndio CHADEMA a.k.a watanzania wanao ishi kwa hofu kubwa sana kwa mujibu wa maneno yao ya mitandaoni.

Kwa mtu asiye ijua Tanzania au anaye ishi nje ya Tanzania akifuatilia kundi hili la CHADEMA wa mitandaoni anaweza kudhani nchi inawake moto.

Ukitaka kundi hili liwe na furaha sana na uitwe mwenye akili kubwa basi unatakiwa useme:

CHADEMA ndio chama bora Cha siasa kuliko vyote barani Afrika.
Lissu ndio mwanasheria bora zaidi kuliko wote Tanzania.
Lissu ndio binadamu pekee mwenye akili nyingi kuwazidi watanzania wote.

Yote tisa kumi, tukana serikali kwa kadiri uwezavyo hapo utakuwa umewakonga nyoyo zao haswaa.
Where is Azory Gwanda, Where is Ben Saanane? Where is Mawazo, What can ou say about dead bodies in the nylon sacs at Coco Beach? (Maiti za sandarus coco beach) etc etc. Kwanini wasiwe na hasira?
 
Haswa safari hii. Yaani wameghairi kabisa kuzungusha mikono na kupiga deki lami. Mgombea wao kila siku analalamika eti ameteguliwa mguu na marisasi sijui nini, upuuzi mtupu.

Kauli kama hizi ni za wale walio panga shambulio lile la mauaji.

Mnasikitika sana hakufa.

Mna roho mbaya sana heri ya majambazi watoa roho za watu.
 
Mbona Mimi sio mpenzi wa Chadema Ila nina hasira sana, nina hasira sababu nyie CCM mnatufanya sisi Watz wajinga mnasema mmejenga viwanda 8000 plus,
Mnasema mmeajiri watu million 6.

Mnasema elimu bure lakini watu wanachangishwa michango mpaka watoto wengine wanaacha shule.

Na mambo mengine mengi ya uongo yamenipa hasira sana.

Note: Sijasoma uzi wote, zaidi nimesoma kichwa cha habari mana kinasadifu yaliyomo.
 
Wafuasi na wapenzi wa CHADEMA. Kwa maoni yangu binafsi kwasasa hapa nchini wafuasi na wapenzi wa CHADEMA ndio kundi la watu wenye Hasira kali zaidi.

Watu hawa wamegawanyika sehemu mbili

1: Tabaka la Uongozi wa CHADEMA. Viongozi wa hiki chama ni watu wenye Hasira kali Sana, Chuki, husuda, visasi

Ukisikiliza hotuba zao utagundua hilo. Ni watu wenye kutamka maneno makali yenye kubeba hisia nzito kutoka mioyoni mwao ambazo wanatamani watanzania wote wawe nazo. Vyama pinzani vyote vingine wanataka viunge mkono CHADEMA kwa chochote kile watacho sema kinyume na hapo basi ni mamluki wa CCM.

Ikitokea siku moja Tanzania kila mtaa unawaka moto, huku watoto wakibakwa kikatili, kuuawa na vilio kila Kona basi siku hiyo kwao itakuwa ni sherehe kubwa sana.

2: Wafuasi na chama, wapenzi na wakeleketwa. Hawa nao ni watu wenye Hasira kali sana, ni watu wenye maneno makali yenye lengo la kuudhi hata pasipo sababu kabisa.

Mfano Mzuri ni hapa jukwaani ole wako ukianzisha mada isiyo sifu CHADEMA tena bahati mbaya iwe na hoja ngumu kujibika zenye ukweli kuhusu chama chao, hapo ndipo hasira huwaka zaidi. Utakutana na kauli za ajabu Kama:

Mataga
Uza ubongo mana unakaa nao kwa hasara.
Lissu amewasika kunako
Huna akili
Pumba n.k

Wakiambiwa na viongozi wao kuhusu kuandamana kudai haki basi hapo hulipuka kwa shangwe kubwa sana wengine hudiliki kusema damu imwagike!

Muda huo wanakuwa wamesahau kuwa.

Yawezekana mumewe au mke ni wa chama kingine tofauti na yeye.

Mwanaye, mjomba, shangazi, boss wake ofisini, jirani yake, mpangaji mwenzake, mfanya biashara mwenzake, rafiki wa familia yake n.k ni watu wa vyama tofauti na yeye. Hajui kwamba akianza kumwaga hiyo damu itaanzia nyumbani kwake kumwagika.

Kwa kifupi hao ndio CHADEMA a.k.a watanzania wanao ishi kwa hofu kubwa sana kwa mujibu wa maneno yao ya mitandaoni.

Kwa mtu asiye ijua Tanzania au anaye ishi nje ya Tanzania akifuatilia kundi hili la CHADEMA wa mitandaoni anaweza kudhani nchi inawake moto.

Ukitaka kundi hili liwe na furaha sana na uitwe mwenye akili kubwa basi unatakiwa useme:

CHADEMA ndio chama bora Cha siasa kuliko vyote barani Afrika.
Lissu ndio mwanasheria bora zaidi kuliko wote Tanzania.
Lissu ndio binadamu pekee mwenye akili nyingi kuwazidi watanzania wote.

Yote tisa kumi, tukana serikali kwa kadiri uwezavyo hapo utakuwa umewakonga nyoyo zao haswaa.
Mimi siku hizi nawaogopa sana Wana CDM maana Wana hasira Kali sana,tena wengine ni Marafiki zangu lakini nawakwepa sana maana kila saa Wana hasira!! Kuna group moja la WhatsApp nilitania kidogo tu kwa kusema, Lissu kasema atahalalisha Ushoga akipata Uraisi! Wwe nilijiwa juu na Wana CDM mpaka admin akanitoa kwa group kwa kua nae ni CDM!
 
e794fdac-23cb-4d1a-a0f5-efb0261ff699.jpg

ukisema mwaka huu damu itamwagika,wajuba wanaendelea na harakati zao kama hivi.maana huna sera.
 
Hasira zipo sana kutokana na utimamu wetu wa kufikiri hivi huu unafiki wa kudai demokrasia ipo wakati haipo unakera pamoja na kauli yenu ya ''mapinduzi daima'' inaashiria mauaji.
 
Na ndio wafuasi wasio Jitambua Dunian sio Tanzania
Yapo yapo kupelekeshwa na Viongozi wao
Hawajui kukosoa kila kitu ni Kufuata mkumbo tu
Wengi ni Domo tu vitendo 0
Wana jipa matumaini hewa kujifurahisha tu
 
Mnafanya mambo ya kipuuzi halafu mnataka tuwachekee! Mimi siyo chadema, ila nina hasira kali sana na nyinyi CCM kwa kutonipandisha daraja tangu mwaka 2015, kisa eti mnanunua ndege!

Hiyo ndege mimi inanisaidia nini!
 
Back
Top Bottom