Wapenzi wa CHADEMA ndio kundi la watu wenye hasira sana kwa sasa

Umeongea facts mzee na utawajua kupitia comment zao hapa.
 
Mnafanya mambo ya kipuuzi halafu mnataka tuwachekee! Mimi siyo chadema, ila nina hasira kali sana na nyinyi CCM kwa kutonipandisha daraja tangu mwaka 2015, kisa eti mnanunua ndege!

Hiyo ndege mimi inanisaidia nini!
Wewe umejuaje mtoa mada Ni CCM?
 
Haswa safari hii. Yaani wameghairi kabisa kuzungusha mikono na kupiga deki lami. Mgombea wao kila siku analalamika eti ameteguliwa mguu na marisasi sijui nini, upuuzi mtupu.
Mbona kuna mgombea badala ya Pushups anacheza Singeli? Hii Sera ya Singeli mnaamini itawasaidia kina mama wa vijijini?
 
Mnafanya mambo ya kipuuzi halafu mnataka tuwachekee! Mimi siyo chadema, ila nina hasira kali sana na nyinyi CCM kwa kutonipandisha daraja tangu mwaka 2015, kisa eti mnanunua ndege!

Hiyo ndege mimi inanisaidia nini!
Mkuu acha unyonge Kama uriziki na Mambo ya Boss wako ya kutokupandisha daraja,si ujiajiri tu alafu ujipandishe mwenyewe Madaraja unayotaka!!
 
Unakataa huku unatenda. Umejibu kwa kukurupuka na jazba halafu unasema huna jazba. Utapasuka moyo bure, wenyewe wanakula ruzuku.
 
Mkuu acha unyonge Kama uriziki na Mambo ya Boss wako ya kutokupandisha daraja,si ujiajiri tu alafu ujipandishe mwenyewe Madaraja unayotaka!!

Mimi siyo mnyonge! Ninachokifanya ni kuidai tu haki yangu ya msingi kama mfanyakazi, kutoka kwa mwajiri asiyejielewa. By the way, hakuna Nchi duniani ambayo wananchi wote wamejiajiri!

Muhimu unapopewa dhamana ya kuwaongoza wengine, unatakiwa utende HAKI! Ukishaanza kuleta mambo ya ubaguzi, jeuri, kiburi, nk. utachukiwa tu.
 
Mimi siyo mnyonge! Ninachokifanya ni kuidai tu haki yangu ya msingi kama mfanyakazi, kutoka kwa mwajiri asiyejielewa.
Sasa ukiona Mwajiri ajielewi,piga chini kazi yake na nenda katafute Mawajiri mwingine au Wwe Jiajiri mwenyewe! Ukiona Mwenye Nyumba anakusumbua na hataki kukusikiliza hasira za nini,tafuta Nyumba nyingine au Jenga yako ili na wwe ujipangie Mashariti yako!! Maisha ni simple sana haitaji hasira!!
 
Kwa hivyo mambo yakienda mrama kwenye nchi yako unahama nchi au unaunda nchi yako?
 
Kuna mda inabidi chuki na hasira iwepo kwa dhuluma za wazi,juzi Maalim Seif kasema mwaka huu wakitugusa kama ni mawe au marungu tutapambana
 
Hivi kama ndugu walikuwa wanawekwa kwenye viroba ,wanatekwa na kupotea na wengine kuuawa kikatili na ni chadema tu usiwe na chuki na hasira ,lissu kapigwa risasi 16 ,mbowe wamefanyia mali zake hujuma hawakutosheka na kumtengua miguu halafu usiwe na huruma na chuki ?

Mimi siyo chuki tu hata wakisema tunoe mapanga nipo tayari
 

Dawa sahihi ya kuondokana na tatizo siyo kukimbia! ni kupambana kulitatua. Mfanyakazi kudai haki yake kwa mwajiri siyo dhambi! Iko duniani kote. Na unapokutana na mwajiri asiyejielewa kama CCM, hasira lazima zitatawala tu.

Huwezi kuninyima haki zangu za msingi kisa unanunua ndege, halafu nikuchekee tu au eti niache kazi ambayo nimeisomea kwa taabu na shida nyingi! Hilo haliwezekani.
 
Where is Azory Gwanda, Where is Ben Saanane? Where is Mawazo, What can ou say about dead bodies in the nylon sacs at Coco Beach? (Maiti za sandarus coco beach) etc etc. Kwanini wasiwe na hasira?
Ndugu zako ni wangapi miongoni mwa makindi uliyotaja
 
Siku ukijiajiri ndiyo utajua kumbe mwanzo ulikua kifungoni!!
Wote tumeajiriwa aidha na muajiri proper au clients wetu, so hiyo dhana ya kujiajiri haipo labda uwe unacheza kamari peke yako.
 
Wewe UVCCM acha na wewe kunipandisha hasira asubuhi yote hii! Hivi inahitaji kuwa na elimu kubwa sana kugundua hata wewe tu uliyeni quote hapa ni CCM?
Kama Ni hivyo unavyohisi kwanini wewe unapinga kwamba sio mshabiki wa CHADEMA?
 
Kama Ni hivyo unavyohisi kwanini wewe unapinga kwamba sio mshabiki wa CHADEMA?

Kuna utofauti kati ya mshabiki na mwanachama. Mimi si mwanachama wa chama chochote kile cha kisiasa! Ni mfuasi tu wa mabadiliko ya kweli ya kuiondoa ccm madarakani.

Hivyo kinapotokea chama chochote kile chenye maono ya kuindoa ccm madarakani, basi moja kwa moja mimi ni mfuasi wao. Including Chadema.
 
Kwanini tusiwe na ghadhabu wakati kuna jitu linafanya mambo ya hovyo hovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…