Wapenzi wa dini tofauti

Si kweli mwanamke wa kiislam hana dini. Usitake mengine humu kisha mseme mambo ya udini. Kwanza sijaona ukristo unasema muoane. Hata Yesu hakuoa!
Mapadre hawaoi. Sijui mnaoana kumfuata nani?
 

Kama unampenda utampa utamlinda
Kila binadamu ktk safari ya maisha yake kuna wakati atatakiwa afanye maamuzi magumu
Kama mwanamke hawezi kubadili dini basi utapaswa uamue moja kati ya kubadili dini umuoe au kumuacha aende.
Sikushauri hata kidogo muoane kila mtu na imani yake.
Ndoa yenye imani moja ni imara zaidi kuliko ndoa ya imani mbili tofauti
 


Sikia nikwambia ndugu yangu

Hilo ni suala very sensitive na inabidi ulichukulie kwa umakini mkubwa.

kwanza, hebu jiulize lengo la uhusiano wenu nini..kaeni pamoja mshauriane nini hasa mnataka...je mwataka kuwa mke na mume, ama mwataka kuwa tu wapenzi kawaida?

Pili, mkishajijibu apo juu, jadilini vikwazo na fursa (obstacles and opportunities) kwenye huo uhusiano..kama ni lengo la ndoa, definately itakuja issue ya dini

Tatu, ijadilini honestly kati yenu, mintarafu faida na hasara za kubadili dini kwa kila mmoja wenu (ikiwezekana mchore kabisa table)

Nne, pimeni faida na hasara hizo, mtaona wazi kwamba nini kinatakiwa. Wakati wa kujadili mjaribu kufikiria muktadha mzima wa mambo ya dini hapa nchini, commitments za kila mmoja wenu kwenye dini, madhara yatakayopatikana ikiwa mtapata watoto...watafuata dini ipi kama hamtakuwa pamoja nk

Tano, wakati mnajadiliana haya jaribuni kuwa wakweli na waaminifu. hapa ninapata mashaka maana mwenzio tayari ameshakuambia ubadili dini...hili halipaswi kuja hivi, linatakiwa lije automatically na sio kwa njia ya msukumo fulani kutoka kwa mwenzio.

So please go and sit down na huyo mwenzio mjadiliane kisha utuletee majibu hapa mmekubalianaje tunaweza kukushauri zaidi.
 
SIKIA kIJANA
jenga msingi wa maisha yako ndani ya yesu.
usithubutu kabisa kumuacha maana huko unapotakakujiunga kisa mapenzi utapotea.
yesu ni mwaminifu atakupa wa kufanana na wewe ,
ubarikiwe mpedwa.
 
Si kweli mwanamke wa kiislam hana dini. Usitake mengine humu kisha mseme mambo ya udini. Kwanza sijaona ukristo unasema muoane. Hata Yesu hakuoa!
Mapadre hawaoi. Sijui mnaoana kumfuata nani?

inawezekana umesema kwa kuwa hujui......
malizia hata paulo hakuoa ila alisema ikishindika na kila mtu awe na mwenza (kutokana na tamaa za mwili)from the bible.
 

Yani usimuache yesu u will regert through out of your life i can guarantee you for 100 perce
 
Huyu mleta sredi ni asherati flani na liacheni lioe mwasherati mwenzake.

hapo unatafuta mtu wa kuwapa wazazi wako wajukuu alafu unaignore ishu ya dini? Kuna wakati mambo huwa magumu na ni dini tu inayoweza kukupa faraja not Madaktari au Specialists yeyote.

Kaka jiondokee Mke mwema hutoka kwa Mola na Mola hukupa wa kufanana naye.
 
NDUGU YANGU NILIKUWA NA TATIZO KAMA LAKO NANIMEDUMU KWA MIAKA MINNE HATIMAYE NIMEAMUA KUTAFUTA INFINITE SOLUTION .WAKATI UNA ANZA MAHUSIANO HILO TATIZO UNAWEZA USILIONE ILA SASA UMRI UNAPOANZA KWNEDA NA MNAPOANZA KUFIKIRIA SUALA LA NDOA NDO UTATA UNAPOANZA KILA MTU ANAVUTIA KWAKE .
USHAURI WANGU KWA KIKFUPI
a)KAMA UNAMPENDA KWA DHATI UTAKI KUMWACHA SIKILIZA ANACHOTAKA
b)ANZA KUMTENGENEZEA MAZINGIRA YA KUFUNGA NDOA YA BOMANI (NOT RECOMMENDED SANA HASA KWA MALEZI YA WATOTO KIDINI)
c)GIVE UP THE FIGHT INGAWA UTAUMIA SANA NA KAMA ALIKUWA ANAKUPENDA ANAWEZA KUUSIKILIZA MOYO WAKE NA KURUDI KUFUATA NJIA YAKO .VINGINEVYO NDUGU HUO NI MGOGORO WA NAFSI NA UTAKUTESA SANA UTASAMBUKA SANA KATIKA MAISHA WAKATI MAPENZI NI FURAHA.
d)ANGALIA MAANUFA YA KUISHI KWA NAYE FOR FUTURE PLAN KABLA UJAA GIVE UP THE FIGHT (TABIA, UWAJIBIKAJI WAKE )
I TOLD YOU FROM EXPERIENCE .
 

usinichukulie muasherati make nimependa kama wengine,labda challenge ninazozipata ndo zinanisumbua akiri ndungu yangu.!
 
Inanikumbusha mtu mmoja wa kwetu mkatoliki alimpenda binti wa shehe. Akaambiwa hakuna kumwoa binti huyo asiposilimu. Jamaa akasilimu akaoa. baada ya miaka minne na watoto wawili, jamaa ameurudia ukristu na mke bado anaye.
 
Mie sikushauri ubadili dini..Lakini mwisho wa siku moyo wako ndio mwamuzi
 
mwanamke hana dini...................., ni mfuasi wa mwanaume utakapoenda nae atakufuata tu

ndoa za mchanganyiko mara nyingi hazina amani zinavuruga watoto wakiwa wadogo na kukosa maadili ya dini moja mwishowe wanaishia kutokuwa na hofu ya Mungu
 
mwanamke hana dini...................., ni mfuasi wa mwanaume utakapoenda nae atakufuata tu

ndoa za mchanganyiko mara nyingi hazina amani zinavuruga watoto wakiwa wadogo na kukosa maadili ya dini moja mwishowe wanaishia kutokuwa na hofu ya Mungu

Mkuu umeongea point ingawa mimi si mshabiki wa dini yeyote.. ila mimi namshauri atafute yule ambaye unafikiri happ baadaye mtakuwa comfortable pamoja.. nikiwa na maana tafuta yule wa dini yako alafu kama wewe una mika 24 yeye atakuwa na mingapi..? wasichana wa kiislam wengi wanatafutiwa wachumba .. mtu mzima unabadili dini yako unaishia imekula kwako.. Nenda church katafute demu.. au walokole wanakupotezea
 



tuachie kichefuchefu mkatoliki gani hata hujui maandiko......au unamwona yesu alikuwa mwehu alipowafundisha wakatoliki...catholics are followers of Jesus Christ...na aliwafundisha hayo kwenye redS...okey fuata hayo yote mawili halafu uone, mnang'ang'ania chuo tu wakati mwingine mjue tamaduni za dini zenu pia...am sorry kwa kuhubiri....AU UNAWEZA KUTUMIKIA MABWANA WAWILI?

I was born with it and not without it
 
Si kweli mwanamke wa kiislam hana dini. Usitake mengine humu kisha mseme mambo ya udini. Kwanza sijaona ukristo unasema muoane. Hata Yesu hakuoa!
Mapadre hawaoi. Sijui mnaoana kumfuata nani?


Wanaojadili mambo ya dini hawaijui dini....wanaoijadili ipi ni njia hawaijui njia na kama dini zisingekuwepo basi Mungu angekuwepo tu.


I was born with it and not without it.
 
Nijuavyo mimi kwa wakatoliki wanaruhusu ndoa za madhehebu mbalimbali (ndani ya ukristo) na hii haihitaji process ndefu ni suala la kumwona Paroko tu atakueleza. Vilevile wakatoliki wanaruhusu ndoa za dini mbalimbali (mkristo na siye mkristo) na anatoa ruhusa askofu wala process siyo ndefu. Ni suala la paroko kuongea na askofu tu. So bado mnaweza kuoana tu kihalali isipokuwa wenzetu kidogo wanapenda kushinikiza (kadili nilivyoexperience) anayetaka kumuoa anu kuolewa na nao abadili imani yake ya kidini.

Nakushauri sana kama mdogo wanu ubaki na imani yako, ninahakika ushapewa kipaimara na kuimarishwa. mshauri mwenzio akitaka kuolewa nawe basi abaki na imani yake na we yako, au kama atakubali kubadili basi abadili (kwa uamuzi wake). Zaidi ya yote mtangulize na mwogope Mungu daima kwa kila ulifanyalo!
 
kama yy binti ndio anakuoa basi badili dini ila kama ww ndio unae oa basi abadili dini kwani anatakiwa akufate ww kama kichwa alafu malia shule kwanza achana na mapenzi kwanza
 
mwanamke hana dini...................., ni mfuasi wa mwanaume utakapoenda nae atakufuata tu

ndoa za mchanganyiko mara nyingi hazina amani zinavuruga watoto wakiwa wadogo na kukosa maadili ya dini moja mwishowe wanaishia kutokuwa na hofu ya Mungu


mkuu rejea hapo kwenye reds...ndoa lengo lake si kupata watoto tu na hilo pia huvuruga amani kama hutapata watoto katika ndoa hilo moja...mbili kuwafundisha watoto wawe na hofu kwa Mungu hapa una maana gani?....the fear of God is the beginning of wisdom.....hapo ni mantiki kama mtapata watoto.

I WAS BORN WITH IT AND NOT WITHOUT IT.
 
wazo la kubadilisha dini ni mwanzo wa ulegevu kiasi kwamba hata wakwe zako watakuwa na nguvu katika ndoa yenu.... Komaa baab we ndo kichwa cha nyumba ukianza kuyumba mwanzo wa safari hiyo ni dalili tosha kuwa umejivua dignity yako...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…