Mimi ni kijana mkatoliki mwenye miaka 24 nina soma chuo mwaka wa tatu,mpenzi wangu ni muislamu anaelimu ya kidato cha nne kwa sasa anaishi na wazazi wake, mausiano yetu ni takribani miaka 2, ktk mazungumzo yetu ananitaka nibadili dini,ila mimi sijalizungumzia hilo kwasababu wazazi wetu wote hatujawafahamisha ila tuna mpango.kubadili dini siwezi na mpenzi wangu siwezi kumuacha,nina pata utata sana, hata sijui nifanyeje ndg zangu?
Sikia nikwambia ndugu yangu
Hilo ni suala very sensitive na inabidi ulichukulie kwa umakini mkubwa.
kwanza, hebu jiulize lengo la uhusiano wenu nini..kaeni pamoja mshauriane nini hasa mnataka...je mwataka kuwa mke na mume, ama mwataka kuwa tu wapenzi kawaida?
Pili, mkishajijibu apo juu, jadilini vikwazo na fursa (obstacles and opportunities) kwenye huo uhusiano..kama ni lengo la ndoa, definately itakuja issue ya dini
Tatu, ijadilini honestly kati yenu, mintarafu faida na hasara za kubadili dini kwa kila mmoja wenu (ikiwezekana mchore kabisa table)
Nne, pimeni faida na hasara hizo, mtaona wazi kwamba nini kinatakiwa. Wakati wa kujadili mjaribu kufikiria muktadha mzima wa mambo ya dini hapa nchini, commitments za kila mmoja wenu kwenye dini, madhara yatakayopatikana ikiwa mtapata watoto...watafuata dini ipi kama hamtakuwa pamoja nk
Tano, wakati mnajadiliana haya jaribuni kuwa wakweli na waaminifu. hapa ninapata mashaka maana mwenzio tayari ameshakuambia ubadili dini...hili halipaswi kuja hivi, linatakiwa lije automatically na sio kwa njia ya msukumo fulani kutoka kwa mwenzio.
So please go and sit down na huyo mwenzio mjadiliane kisha utuletee majibu hapa mmekubalianaje tunaweza kukushauri zaidi.