Jamani mimi napenda kuangalia movie za kutisha zinazohusisha wanyama na binadamu (horror adventures) sio za kikatili za binadamu kwa binadamu.
mwenye kuzijua naomba anitajie.
Kuna moja siijui jina ila kuna baba mmoja ana watoto wawili k na m, baada ya kuacha na mkewe akao mke mwingine sasa wakenda fungate pamoja na watoto wao kwenye mbuga ya wanyama, mtoto wa kike ambaye ndiye mkubwa alikuwa hampendi kabisa mama yake mdogo kwa kuamini kuwa ndiye aliyesababisha mama yao kuachwa. basi wakiwa huko kwenye fungate baba yao aliwaambie waende na mama yao kuangalia wanyama basi wakiwa wao (watoto na mama yao na dereva) yule wa kiume alibanwa haja ndogo ikabidi wasimame mahali ambapo si salama,
akashuka dereva na mtoto wa kiume(dereva alizima gari akashuka na funguo) ndani ya gari alibaki mama mdogo na mwanaye wa kike) ....
wakati kijana anajisaidia mara simba ................. kijana alipona baada ya kukimbia lakini dereva aliraruliwa na simba na historia ya maisha yake ikaishia pale, songombingo ndipo lilipoanzia gari imezimwa funguo walipokuja kuiona kwa kutumia darubini ndipo kulipo na simba..................., kabla ya kufikia wokovu .............. jinsi wawindaji wawili walivyoraruliwa na simba, .................. jinsi yule baba aliyemsindikiza baba yao alivyouawa na simba na mateso waliyoyapata hata mwisho wakawa familia moja yenye upendo. so sad...........
Jurasca park, the shark, Clocodile, na zifafanazo
Jamani kuna moja mwenye kuijua naomba anitajie, maana nilikuwa mdogo ila kuna baadhi ya scne nazikumbuka kuna baba mmoja alikua anaishi nje ya mji na familia yake basi siku moja akiwa anacheza golf na kijana wake kitenis kikaenda kuangukia kwenye samba la mahindi alipoenda kukifuata akamona baba mmoja kisha yule baba akapotea, yule baba akabaki anashanga kisha akarudi na kitenis.
siku moja akenda mjini kuhemea, mara buchani muuz nyama ni yule mtu aliyemuona kule shamba akataka kuongeza mara yule baba akamwambia so what, akapotea, yule baba akatoka akaenda kwenye nyanya akamka tena yule ghost, maskini baba wa watu akaanza kuchanganyikiwa akatoka akapanda gari arudi nyumbani akakuta anayeongoza magari ndiye yule ghost akataka kusema kitu yule ghost akamjibu so what.......... kwa jinsi picha ilivyokuwa na vitimbi mwenyewe ilinitisha sikuimaliza ila leo natamani niiangalie, mwenye kujijua please...
Nyingine ya kitoto inaitwa CASPER mwenye kuijua kama ninaweza kuidownload please.