Wapenzi wa push-ups & squats

Wapenzi wa push-ups & squats

Salaam wakuu na hongereni kwa kushiriki vita ya kuitokomeza corona

Katika kuweka mwili fiti nimeona Kuna mazoezi mawili yasiyohitaji eneo kubwa, na hata chumbani unaweza kuyafanya, nayo Ni pushups kwa kujenga mwonekano wa juu wa mwili , na squarts kwa kujenga mwonekano wa chini wa mwili

Wapenzi wa mazoezi hayo karibuni mtuambie ulianzaje kupiga push-ups na unamudu kupiga pushups ngapi, squats ngapi na utimamu wa mwili wako ukoje.

Karibuni
Ninatetemeka mikono kila nikipiga push ups! Yaani najikuta kuna nyakati nashindwa kushika kijiko
 
Siku hiz napiga push up 120 kila asubuhi.

Napiga 30 30 napumzika mpaka zinafika 120
Nimekuwa inspired.
 
Kawaida tuna push ups za aina tatu yaan
1) diamonds push-ups
2) narrow push-ups
3) wide push-ups

Jitahidi atleast kwa siku jumla ya hizo pair tatu upige ata 75 tu inatosha,
Ukipiga hizo zote kwa pamoja utatanua kifua mbavu na mabega
 
Push up Ni zoezi zuri...

Anza pale ulipo...halafu Hakikisha unajichalenge mwenyewe kila siku..

Mfano leo ukipiga tano.. kesho piga Saba, keshokutwa 8,

Hakikisha unaizidi Jana...

Utakaa sawa TU...
Mimi nilianza na Saba....
Ila Sasa nakimbiza 50+ mzunguuko mmoja
Hongera sana
 
Push up Ni zoezi zuri...

Anza pale ulipo...halafu Hakikisha unajichalenge mwenyewe kila siku..

Mfano leo ukipiga tano.. kesho piga Saba, keshokutwa 8,

Hakikisha unaizidi Jana...

Utakaa sawa TU...
Mimi nilianza na Saba....
Ila Sasa nakimbiza 50+ mzunguuko mmoja
Ahsante kwa ushauri kuhusu push up.Awali nilikuwa naogopa kupata masugu mikononi mkuu.
 
Back
Top Bottom