Habari za jioni wakuu.
Nakumbuka wakati nipo Dar nilikuwa mpenzi mkubwa wa kutembelea rooftop bars ama restaurants.
Kila mwezi nilipendelea sana kutembelea aidha Holiday inn roof top, Harbor view roof top, New African Hotel roof top na zingine.
Nilipenda sana mandhari hizi kwa sababu zilikuwa ni tulivu na unapata huduma kwa thamani ya fedha yako. Ingawa baadhi ikifika mida ya night kali zinavamiwa na changudoa na kuharibu/kukoleza taswira halisi ya sehemu husika.
New Africa restaurant walikuwa na chef mahiri sana na msosi wao ulikuwa wa uhakika sana, mwanga hafifu na huduma bomba sana. Taswira ya mwanga unaoangazia bandarini na meli zinazopakuwa mizigo nyakati za jioni zinakupa view moja matata sana.
Harbor view roof top pembeni ya ile swimming pool unaweza kumaliza hata vikombe kumi vya kahawa na ukaendelea tu kutulia, ingawa sometimes panavamiwa na dada poa wa kichina wanaotegesha pale chini Grand casino.
Holiday Inn kila alhamisi roof top kunanoga kwa nachi za kiarabu, na jamaa wa pale bar ni mjuzi sana wa kuchanganya cocktail za kufa mtu ingawa napo sometime panafurika changu.
Wewe ni shabiki wa rooftop gani? Karibuni leta ushuhuda wako.
cc
GuDume Mshana Jr ,
Sky Eclat