Wapenzi wa rooftops (migahawa na kumbi zilizopo juu ghorofani) njooni hapa

Wapenzi wa rooftops (migahawa na kumbi zilizopo juu ghorofani) njooni hapa

Ni maeneo kama haya ndio unaweze kufahamiana na wapiga dili wakubwa ama wafanyabishara wakubwa na maofisa wakubwa wakubwa tu. Mi nilivyoanza kumu introduce jamaa yangu mmoja kwenye hizi rooftops nilianza na pale Holiday Inn, kwa bahati kulikuwa na semina pale na kulikuwa na wageni, jamaa ali enjoy sana alikutana na kisu kimoja toka UNDP dada baada ya kupiga vyombo alihitaji huduma ya siri jamaa yangu akamchangamkia, kwa msaada wa huyo dada jamaa yangu alipata kazi nzuri tu. Roof top zina heshima yake.
 
Habari za jioni wakuu.

Nakumbuka wakati nipo Dar nilikuwa mpenzi mkubwa wa kutembelea rooftop bars ama restaurants.

Kila mwezi nilipendelea sana kutembelea aidha Holiday inn roof top, Harbor view roof top, New African Hotel roof top na zingine.

Nilipenda sana mandhari hizi kwa sababu zilikuwa ni tulivu na unapata huduma kwa thamani ya fedha yako. Ingawa baadhi ikifika mida ya night kali zinavamiwa na changudoa na kuharibu/kukoleza taswira halisi ya sehemu husika.

New Africa restaurant walikuwa na chef mahiri sana na msosi wao ulikuwa wa uhakika sana, mwanga hafifu na huduma bomba sana. Taswira ya mwanga unaoangazia bandarini na meli zinazopakuwa mizigo nyakati za jioni zinakupa view moja matata sana.

Harbor view roof top pembeni ya ile swimming pool unaweza kumaliza hata vikombe kumi vya kahawa na ukaendelea tu kutulia, ingawa sometimes panavamiwa na dada poa wa kichina wanaotegesha pale chini Grand casino.

Holiday Inn kila alhamisi roof top kunanoga kwa nachi za kiarabu, na jamaa wa pale bar ni mjuzi sana wa kuchanganya cocktail za kufa mtu ingawa napo sometime panafurika changu.

Wewe ni shabiki wa rooftop gani? Karibuni leta ushuhuda wako.

cc GuDume Mshana Jr , Sky Eclat
Asante kwa kuanzisha huu uzi kuntu mkuu. Mm binafsi ni mshabiki wa roof tops na mojawapo ya roof tops nilizowahi kuwepo ni roof top moja ipo pale mtaa wa buguruni sheli ila pale wakati wa kuanzia saa 12:30 jioni panafurika vyanguduo hatari sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Brother tpaul siku nyingi sijapita maeneo hayo pale Buguruni sheli unaongelea hotel gani pale? kuna hii moja ipo mkono wa kushoto kama unatokea sokoni. Ni ya gorofa hivi lakini sidhani kama kuna roof top pale, inataka umakini kidogo maana mida ya jioni inazungukwa na wamachinga wa buguruni. Nimewahi kufika sana pale, mida za jioni kuangalia EPL lakini mbu walinifukuza.
 
Brother tpaul siku nyingi sijapita maeneo hayo pale Buguruni sheli unaongelea hotel gani pale? kuna hii moja ipo mkono wa kushoto kama unatokea sokoni. Ni ya gorofa hivi lakini sidhani kama kuna roof top pale, inataka umakini kidogo maana mida ya jioni inazungukwa na wamachinga wa buguruni. Nimewahi kufika sana pale, mida za jioni kuangalia EPL lakini mbu walinifukuza.

Mkuu kuna roof top moja ya asili--ipo opposite na Buguruni shell upande wa kushoto wa barabara ya kwenda Ubungo --imepakana na jengo moja la hotel (nimeisahau jina). Yaani ukitoka Kimboka (uwanja wa vyangudoa) unatembea kama hatua 80 unafika mahali hapo. Roof top yenyewe sio kali kiviiile--ni ya kiswahili zaidi--inawafaa wananchi wa kima cha chini na kati.
 
Sawa sawa mkuu one day tunaenda kupaona
 
94FDA0CD-416F-4DF1-92B1-56A9646A0D11.jpg
 
Huko ni kwa wastaarabu tu, ...wale wasiopenda kuondoka hadi waanzishe ugomvi hapawafai.
 
Back
Top Bottom