Wapenzi wa rooftops (migahawa na kumbi zilizopo juu ghorofani) njooni hapa

Wapenzi wa rooftops (migahawa na kumbi zilizopo juu ghorofani) njooni hapa

Muweke na bei jamani, maana hilo ndio la msingi..
Mkubwa Tater wala hakuna gharama za hivyo, ukitoa usafiri wa kukufikisha eneo husika hata 50k unaweza kuenjoy inategemea umeenda na nani na unakunywa/kula nini. Mi kwa kawaida sikuwa na kampani yyte nilikuwa tu mwenyewe na mawazo yangu kichwani. Kwa hio mpaka ninaondoka eneo husika 80K ama 60K inakuwa imeungua. Msosi ndio unakuwa unanigarimu sana maana nipo too much selective.
 
Sky hotel Ramada ila nilikuwa navizia sana muda wa happy hour navizia monde za kitonga.
 
Mkuu Kaizer mimi mzee kuliko wewe na naenjoy kweli, Fanya siku uende
 
Habari za jioni wakuu.

Nakumbuka wakati nipo Dar nilikuwa mpenzi mkubwa wa kutembelea rooftop bars ama restaurants.

Kila mwezi nilipendelea sana kutembelea aidha Holiday inn roof top, Harbor view roof top, New African Hotel roof top na zingine.

Nilipenda sana mandhari hizi kwa sababu zilikuwa ni tulivu na unapata huduma kwa thamani ya fedha yako. Ingawa baadhi ikifika mida ya night kali zinavamiwa na changudoa na kuharibu/kukoleza taswira halisi ya sehemu husika.

New Africa restaurant walikuwa na chef mahiri sana na msosi wao ulikuwa wa uhakika sana, mwanga hafifu na huduma bomba sana. Taswira ya mwanga unaoangazia bandarini na meli zinazopakuwa mizigo nyakati za jioni zinakupa view moja matata sana.

Harbor view roof top pembeni ya ile swimming pool unaweza kumaliza hata vikombe kumi vya kahawa na ukaendelea tu kutulia, ingawa sometimes panavamiwa na dada poa wa kichina wanaotegesha pale chini Grand casino.

Holiday Inn kila alhamisi roof top kunanoga kwa nachi za kiarabu, na jamaa wa pale bar ni mjuzi sana wa kuchanganya cocktail za kufa mtu ingawa napo sometime panafurika changu.

Wewe ni shabiki wa rooftop gani? Karibuni leta ushuhuda wako.

cc GuDume Mshana Jr , Sky Eclat
Pamenivutia kwa uwepo wa machangu
 
wakati ule akitawala mfalme Kaisari, na Herode akiwa Liwali. zamani sana

kwa taarifa zaidi ndugu yangu wa karibu ni babu Asprin...yaani tumebaki hawa watoto wabichi kama kina espy tunawaangalia tu
Ungeniangalia tu si ningefurahi.
 
wakati ule akitawala mfalme Kaisari, na Herode akiwa Liwali. zamani sana

kwa taarifa zaidi ndugu yangu wa karibu ni babu Asprin...yaani tumebaki hawa watoto wabichi kama kina espy tunawaangalia tu
Naam, ndugu yangu. Hakika mwenye macho hajapata kuona na mwenye masikio hajapata kusikia
 
Katib Mkoa naungana na son_of_masia maisha yanatofautiana sana sana. Wewe umejikaza unatumia 80000, anakuja mtu anaagiza chupa ya wine ya dola 350 tena hana habari kabisa. Maana kuna wengine kuweka shilings kwenye wallet ni mzigo ni mwendo wa foreign currency tuu
 
Back
Top Bottom