Wapi dar naweza pata dentist mzuri.

truegooner

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2014
Posts
779
Reaction score
338
Habari. Mi ni mkazi wa Dar es salaam. Nina meno mawili ya juu mabovu (moja incisor na lingine linalofuata kwenda ndani baada ya hilo incisor), yametoboka. Nimewahi kuwa na meno mengine mawili mabovu 2005 yaliyotoboka. Nilifanikiwa kuyaziba nchi jirani muda huo na mpaka leo hayanisumbui. Ila nimeng'oa ng'oa meno ka 2 hivi. Haya niliyong'oa yalianza kwa kutoboka. Nilienda yaziba kwa dentist wawili tofauti hapa Dar, 2009 na 2012. Ila kila walipoziba, baada ya miezi kadhaa yanazibuka tofauti na yale niliyoziba nchi jirani. Kuna watu wananiambia hapa Dar waliziba kwa 'cement' na huko nchi jirani walikuziba kwa 'risasi'. Sasa jamani, kama kuna dentist yeyote mnayemjua ambaye ni mzuri na pia kama anaziba kwa kuweka hiyo risasi itakuwa nzuri zaidi anifaamishe, maana haya meno niliyoweka risasi 'hayanisumbui' kabisa. Nataka nikayashughulikie kabla hayajaanza kunishughulikia. Moja nataka kulitoa kabisa maana lishavunjika vunjika na moja nataka liziba kwa risasi. Kama nitafaamu na bei itakuwa nzuri zaidi. Asanteni.
 
Nenda external hapo ubungo kuna dr anaitwa duke. ni mtaalam hata me kanisaidia. mcheki 0715147509
 
Asante sana mkuu, nitamtafuta huyo Dr.
 
ZAMU INTERNATIONAL walikuwa Regency estate nadhani wamehamia my fair Plaza
 

Kuna mchaga mmoja anaitwa akim yupo pale kariakoo msimbaz karibu na big bon yuko poa sana. Kaweke apointment ujaribu kumuona yupo poa sana ni ghali ila anatibu kisasa sana...ukipata nafasi pitia pale utakuta wahindi wamejazana usikate tamaa omba appointment
 
Nenda Muhimbili mkuu.kuna huduma za binafsi au za umma.unapewa daktari bingwa.kuna madokta wazuri siku hizi hawang'oi meno kama hayajaoza sana wanakufanyia root canal.Dental department yao hakuna usumbufu kama vitengo vingine na gharama ni nafuu.Msiogope jina.Si kila kitu Muhimbili ni kibaya.
 
pole japo hospital hakuna dawa ya tatizo lako ndiomaana umeenda huku nahuko utaishia kungoa na risasi
 
japo ukiona kote wameshakuyeyusha unipm nikusaidie maana usipoangalia meno yote utayamalizia chini, hospital hakuna dawa ya jino liloshambuliwa na wadudu zaidi yakulingoa kukuondolea maumivu otherwise risasi mwisho wa risasi nikungoa, pole nitatizo hilo.
 
mimi kuna jino langu niliziba Kairuki hospital,ilikuwa kama miaka minne iliyopita..Nashukuru nimekaa nalo mda mrefu bila kunisumbua,ingawa mwezi uliopita limetoboka tena,ila nina mpango wa kwenda kuziba tena kwa Kairuki coz wako poa sana
 
mimi meno yangu yameungua.
.. nasikia inawezekana yakawa meupee
kwa baadhi ya dentists centres
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…