truegooner
JF-Expert Member
- Apr 23, 2014
- 779
- 338
Habari. Mi ni mkazi wa Dar es salaam. Nina meno mawili ya juu mabovu (moja incisor na lingine linalofuata kwenda ndani baada ya hilo incisor), yametoboka. Nimewahi kuwa na meno mengine mawili mabovu 2005 yaliyotoboka. Nilifanikiwa kuyaziba nchi jirani muda huo na mpaka leo hayanisumbui. Ila nimeng'oa ng'oa meno ka 2 hivi. Haya niliyong'oa yalianza kwa kutoboka. Nilienda yaziba kwa dentist wawili tofauti hapa Dar, 2009 na 2012. Ila kila walipoziba, baada ya miezi kadhaa yanazibuka tofauti na yale niliyoziba nchi jirani. Kuna watu wananiambia hapa Dar waliziba kwa 'cement' na huko nchi jirani walikuziba kwa 'risasi'. Sasa jamani, kama kuna dentist yeyote mnayemjua ambaye ni mzuri na pia kama anaziba kwa kuweka hiyo risasi itakuwa nzuri zaidi anifaamishe, maana haya meno niliyoweka risasi 'hayanisumbui' kabisa. Nataka nikayashughulikie kabla hayajaanza kunishughulikia. Moja nataka kulitoa kabisa maana lishavunjika vunjika na moja nataka liziba kwa risasi. Kama nitafaamu na bei itakuwa nzuri zaidi. Asanteni.