Wapi dr Luis Shika na kiki zake?

Wapi dr Luis Shika na kiki zake?

Mtarban

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2015
Posts
3,858
Reaction score
5,101
Huyu jamaa yuko wapi mbona kapotea haraka kusikojulikana? Meneja wake atoe majibu haraka tujue jamaa yetu yiko wapi na nini kimemsibu maana tulitegemea msimu huu wa sikukuu angemuandalia tena show kama ile usiku wa 900 itapendeza
 
Hivi baada ya kuwatumia jamaa zile dola 100 ameshaongea chochote kuhusu mustakabali wa hela zake?
 
Na manager lazima atakuwa ameingia mitini, ndio ujue wabongo ni noma wanapenda ready made...mzee alivyotingisha tu bidada akawa manager wake na sasa hivi amefifia tegemea kusikia kila mtu yupo kivyakevyake
 
Huyu jamaa yuko wapi mbona kapotea haraka kusikojulikana? Meneja wake atoe majibu haraka tujue jamaa yetu yiko wapi na nini kimemsibu maana tulitegemea msimu huu wa sikukuu angemuandalia tena show kama ile usiku wa 900 itapendeza
Huyo tangu alivoisapoti chama chakavu ndo kwisha habari yake km original komedi vile,
 
Yule mzee ni mpuuzi sana.
Aliharibu taswira yake ghafla baada ya kujiingiza kwenye kampeni za kisiasa tena za kuisifia CCM. Hapo ndipo wabongo walipomtema ghafla. CCM ni laana na nuksi kubwa. Yule mzee ndio kajichimbia kaburi, hawezi kuibuka tena.
 
Huyu jamaa yuko wapi mbona kapotea haraka kusikojulikana? Meneja wake atoe majibu haraka tujue jamaa yetu yiko wapi na nini kimemsibu maana tulitegemea msimu huu wa sikukuu angemuandalia tena show kama ile usiku wa 900 itapendeza
Umaarufu wake uliisha baada ya uchaguzi wa madiwani.Hapana chezea CCM
 
Nilipoona kashikwa mkono na yule aliyepewa chupa ya Maji na Zakhia Meghji nikajua basi tena.
 
Alipoanza kujihusisha na siasa za ccm kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani ndipo alipojiroga na kuanza kupotea kwenye masikio ya watu
 
Yule mzee ni mpuuzi sana.
Aliharibu taswira yake ghafla baada ya kujiingiza kwenye kampeni za kisiasa tena za kuisifia CCM. Hapo ndipo wabongo walipomtema ghafla. CCM ni laana na nuksi kubwa. Yule mzee ndio kajichimbia kaburi, hawezi kuibuka tena.
Taswira gani hiyo aliyokuwa nayo?
Ya kuwaongopea wa tz kuwa ana mabilion hadi watu na heshima zao humu wakujiita wachambuzi na wana intelijensia kila siku wanafungua thread wakimsifu kuwa ni CIA.
Haki Tanzania bila vituko kama hivi vya kupunguza stress tungeshakufa.
Wengine eti wakadai ateuliwe awe waziri wa nishati na madini
 
Amekwishatumika hivyo hahitajiki tena
Naona kama kuna muendelezo (Pattern) fulani hivi. Yule msanii Marlaw alilalamika kwamba kushiriki kwake kwenye kampeni (CCM) kulimmaliza kisanii. Wanaume TMK msambaratiko wao ulianzia baada ya Kampeni za mwaka 2005.

Kina Aslay na mkubwa na wanawe tuliwaona kwenye majukwaa ya CCM, baada ya hapo imebaki Historia. Bongo Movie walikuja na "mkanye Mwanao" lakini leo tunaona jinsi kina Steve Nyerere wakijitahidi kuirudisha kwenye chati Bongo Movie lakini imeshindikana hata kwa maandamano yaliyopokelewa na Makonda.

Nakumbuka zama zile kina Masanja na Kundi lao la "The comedy Show" kabla halijawa "The comedy Original" walivyoteka nyoyo za watanzania. Siku ya Alhamisi ilikuwa ni maalum sana kwa baadhi ya familia kukaa pamoja na kuangalia show hiyo. Lakini imeshakuwa zilipendwa.
 
Back
Top Bottom