Habari?
Sina hakika kama kuna uzi unao elezea hili.
Magari haya tunayo tununua kutoka Japan nk. Mara nyingi huwa tunakuta funguo maja tu.
Lakini naamini kuna mahali funguo ya pili huwekwa / hufichwa ili atakaye inunua aje aikute hapo.
Swali: Je ni wapi huwa wanaziweka / kuzificha / kuzihifadhi?
Mwenye kujuwa tafadhali atufahamishe.
Naomba kiwasilisha.
-----
D.
Nimefurahi kuwa nawe unajuwa hili.Ni kweli huwa kuna mda wanaficha ingawa sijafanya utafiti sana maana kuna kipindi niliwahi kuta funguo kwenye gari aina ya premio kwenye cabinet ya upande wa kushoto kwenye dashboard siti ya mbele. Tuliitoa ile cabinet tukakuta funguo imewekwa pale kwa gundi kabsa