BLUE BALAA
JF-Expert Member
- Nov 30, 2010
- 1,222
- 776
huyu jamaa ni entertainer acha mchezo,jd wa redioni sio wa club!anaipenda kazi yake kutoka damuni na ana displine ya kazi haswa,pamoja na kazi ya u dj hatumii kilevi! Nafikiri imemsaidia kudumu kwenye kiwango chake

Ni kwelo alikuwa DJ mzuri sana and its true huyu bwana hatumii kilevi, there was a time alikuwa analeta wasanii sana Arusha. Yeye ni mtu wa juice tu.

Siyo early 2000 ila ni kati ya maDJ wa mwanzo RADIO ONE miaka ya 1995 kuja 1999.
huwa nasikitika sana baadhi ya madj maarufu sana wa zamani wanapiga muziki kwenye mabaa ya mitaani tena kwa ujira mdogo sana na wakionekana wamechoka kabisa,mmoja yuko palee fairway tegeta,nafikiri mnamfahamu!

nani huyo?
Kuna kipindi cha Love and dedication pia alikuwa akipiga R&B east africa Radio. Jamaa ni mkali sana katika mixing za muziki yaani ngoma zinapandana utashaangaa umecheza miziki mitano bila kujua.. Jamaa ni mkali aisee ni kati ya Ma-Dj wakali Nchini ambao hawatosahaulika!!mnakumbuka mtaa wa mangoma pale radio one enzi zilee Dj JD na fast eddy?
oi! Hiyo kali kwa hiyo amehamia fan nyingineHuyu dj namkubali sana na miss sana pia, ila kuna bibi kizee mmoja wa benki kuu hapo teni milambo amemuweka ndani naona alimuwekea limitation kwenye mambo ya muziki, jamaa kwa njaa zake akaachana na muziki akaamua kufugwa na bibi kizee.
Kulikuwa na Mike Mhagama,Misanya Bingis n.k Vicky Msina!
Ramnkin Ramadhan alikuwa Mtoto wa Kibopa Fulani na Alikuwa Sauti Nzito nzito ya ''Kilevi'' U ahmada ulimtoa kwenye fani
John Dillinger Matlou kama niliwahi sikia mzazi wake mmoja alikuwa ni Mkimbizi wa Saouth Africa pindi zile
Na hilo jina sijui alilipaa vipi kwani John Dillinger wa ukweli alitikisa America miaka ya zamani akaitwa Public Enemy the most Wanted Man In United States Of America
Kulikuwa na Mike Mhagama,Misanya Bingis n.k Vicky Msina!
Ramnkin Ramadhan alikuwa Mtoto wa Kibopa Fulani na Alikuwa Sauti Nzito nzito ya ''Kilevi'' U ahmada ulimtoa kwenye fani
John Dillinger Matlou kama niliwahi sikia mzazi wake mmoja alikuwa ni Mkimbizi wa Saouth Africa pindi zile
Na hilo jina sijui alilipaa vipi kwani John Dillinger wa ukweli alitikisa America miaka ya zamani akaitwa Public Enemy the most Wanted Man In United States Of America

Ni kweli kabisa baba yake alikuwa ni mmoja kati ya wakambizi wa Africa kusini walipewa makazi pale mazimbu Morogoro (Mambweni ya wanafunzi 1st year wa SUA kwa sasa)

Akiwa pale mzee Dilinga Matlou alikutana na mama wa kiruguru na John akazaliwa,

Baadae wale wakimbizi akiwemo Baba wa John Dillinga walirudishwa S. Africa, lakini baba wa John nalikuwa na mawasiliano ya karibu na mama John na hivyo wakati fulani DJ JD akiwa bado mdogo alimfuata baba yake S.africa alisoma huko na baadae kurudi Tanzania.

Akiwa huko S. africa alijifunza kidogo muziki lakini baada ya kurudi huku Tanzania alikutana na mjomba wake ambaye alikuwa DJ pale Morogoro Hotel ukumbi wa shimoni. kuanzia hapo ndipo DJ JD alipoanza kujifunza U-DJ kwa hali na mali na baadae kwa kushirikia na DJ sweet Coffee banana alimudu kupiga Disko hapo Morogoro hotel, Bwalo la Umwema, Rock garden na pale Masuka village na kuteka kabisa umati wa wapenda kwanja Morogoro.

Kwahiyo Mzee Dilinga alikuwa mkimbizi au mmoja wa wapiganaji wa ANC? Pia kuna jamaa aliwahi niambia mama john ni msukuma wa Mwanza ila juhudi kubwa za john Dilinga kupromoti wasanii na muziki wa morogoro inafanya niamini ana asili ya morogoro.Afande sele ni moja ya wasanii aliowapa promo kubwa enzi hizo.Wasanii wana muheshimu kwa kutowadai malipo akipiga nyimbo zao na mara nyingi akipenda nyimbo yako hata kama hakujui anaipiga na mfano ni Latifa ya Mb dog ambayo radio zote madj waligoma kuipiga wakiiona chai tu mpaka alipoanza kuipiga kwa mixing kali ndo mb dog akaanza kutafutwa apeleke single yake na madj wakasahau walishapelekewa ila ipo kapuni!
Huyu dj namkubali sana na miss sana pia, ila kuna bibi kizee mmoja wa benki kuu hapo teni milambo amemuweka ndani naona alimuwekea limitation kwenye mambo ya muziki, jamaa kwa njaa zake akaachana na muziki akaamua kufugwa na bibi kizee.

DJ JD nakumbuka mara ya mwisho nilimuona Mwanza mwishoni mwa Mwaka jana alialikwa kupiga show Stone Club Mwanza Hotel.
Huyu jamaa si alioa binti wa mkubwa mmoja hapa Dar es Salaam, hilo la kuwekwa ndani nina wasi wasi nalo