Ni kweli kabisa baba yake alikuwa ni mmoja kati ya wakambizi wa Africa kusini walipewa makazi pale mazimbu Morogoro (Mambweni ya wanafunzi 1st year wa SUA kwa sasa)

Akiwa pale mzee Dilinga Matlou alikutana na mama wa kiruguru na John akazaliwa,

Baadae wale wakimbizi akiwemo Baba wa John Dillinga walirudishwa S. Africa, lakini baba wa John nalikuwa na mawasiliano ya karibu na mama John na hivyo wakati fulani DJ JD akiwa bado mdogo alimfuata baba yake S.africa alisoma huko na baadae kurudi Tanzania.

Akiwa huko S. africa alijifunza kidogo muziki lakini baada ya kurudi huku Tanzania alikutana na mjomba wake ambaye alikuwa DJ pale Morogoro Hotel ukumbi wa shimoni. kuanzia hapo ndipo DJ JD alipoanza kujifunza U-DJ kwa hali na mali na baadae kwa kushirikia na DJ sweet Coffee banana alimudu kupiga Disko hapo Morogoro hotel, Bwalo la Umwema, Rock garden na pale Masuka village na kuteka kabisa umati wa wapenda kwanja Morogoro.

Kwahiyo Mzee Dilinga alikuwa mkimbizi au mmoja wa wapiganaji wa ANC? Pia kuna jamaa aliwahi niambia mama john ni msukuma wa Mwanza ila juhudi kubwa za john Dilinga kupromoti wasanii na muziki wa morogoro inafanya niamini ana asili ya morogoro.Afande sele ni moja ya wasanii aliowapa promo kubwa enzi hizo.Wasanii wana muheshimu kwa kutowadai malipo akipiga nyimbo zao na mara nyingi akipenda nyimbo yako hata kama hakujui anaipiga na mfano ni Latifa ya Mb dog ambayo radio zote madj waligoma kuipiga wakiiona chai tu mpaka alipoanza kuipiga kwa mixing kali ndo mb dog akaanza kutafutwa apeleke single yake na madj wakasahau walishapelekewa ila ipo kapuni!