Katika kijiji nilipo kule Lupembe, kuna eka zaidi ya 2000 zinauzwa na watu tofauti, mashamba haya nilishiriki kuyapima na kuyanunua, project yetu ya awali ilikuwa miti ya mbao, janga la moto lilikatisha watu tamaa sana wamekimbia na sasa wanauza ardhi kwa wengine.Usiseme hivyo mkuu! Penye nia pana njia. Muhimu ni uvumilivu na kuwa na muda wa kutosha "kupeleleza"
Niliambiwa na zaidi ya watu wawili wa Njombe kuwa kuna "mapori" yanayouzwa shilingi laki moja na hamsini vijiji vya mbali. Walioniambia ni watu wa kuaminika, mmoja wao ni "bilionea" wa maparachichi.