Wapi kwenye katiba imeainisha mapinduzi mazuri na yale mabaya? CCM ina uhalali gani wa kutamba na mapinduzi yake?

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,809
Reaction score
6,948
Kama tunakubaliana kuwa kupanga au kutekeleza mapinduzi ya kisiasa ni uhaini na ni kosa kubwa katika nchi, hatuwezi kusema mapinduzi fulani ya kisiasa ni halali na mengine ni haramu.

Vilevile, hatuwezi kusema kundi fulani la watu lina haki ya kufanya mapinduzi na wengine hawana haki hiyo.

Miaka yote hii CCM, kinachojiita Chama Cha Mapinduzi kimetamba kwamba wao ni wanamapinduzi na hadi msajili wa vyama vya siasa hajawahi kuwaita kuwahoji kuhusu mapinduzi yao.

Leo mwanasiasa wa upinzani akisimama jukwaani akasema anaandaa mapinduzi, ataozea jela. Je, neno mapinduzi linahodhiwa na wanasiasa wa chama fulani pekee mbele ya mkono wa sheria?

Nyerere aliwahusia vijana waasi mifumo kandamizi, halikuwahi kuwa tatizo zaidi ya kuenziwa kama Baba wa Taifa. Leo, watu wanaenzi maneno ya Baba yao kwa kuwaambia wananchi waasi mifumo kandamizi na mibovu ya uchaguzi, wanafunguliwa kesi za uhaini na wanasheria wanapekua kurasa za kamuzi za BAKITA kutafsiri maana ya uasi.

Hili limekaaje kitaalamu na kisheria?
 
Hii ni maada fikirishi kweli ambayo wengi hasa wenye chama chao hawaifikirii kabisa

..Mapinduzi ya Zanzibar ya Jan 12, 1964 yalikuwa ni UHAINI.

..Serikali iliyopinduliwa ilikuwepo kwa mujibu ya Katiba ya Zanzibar.

..neno " mapinduzi " ktk jina la Ccm ni kuenzi yaliyotokea 1964, ambayo ni uhaini.

..kwa hiyo ni sawa kabisa kusema Ccm ni chama cha uhaini / mapinduzi.
 
🤣🤣
 
Ni hatari sana
 
CCM chama cha makanjanja hawawezi kuelewa hilo.
 
..Mapinduzi ya Zanzibar ya Jan 12, 1964 yalikuwa ni UHAINI.

..Serikali iliyopinduliwa ilikuwepo kwa mujibu ya Katiba ya Zanzibar.

..neno " mapinduzi " ktk jina la Ccm ni kuenzi yaliyotokea 1964, ambayo ni uhaini.

..kwa hiyo ni sawa kabisa kusema Ccm ni chama cha uhaini / mapinduzi.
Halafu Bibi Titi waliyemtuhumu kwa uhaini mwingine, wakamuenzi kwa kumpa hadi barabara kwa jina lake na kama nakumbuka vizuri Chifu Hangaya alipoingia, lilifanyika tukio la kumuenzi hiyo muhaini.

Historia ya Tanzania imechakachuliwa beyond repair.
 
Wakati wa Utawala wa Nyerere na Huu wa Samia ni Nyakati mbili Tofauti japo Chama vhao ni Kimoja.
Ndiyo ambavyo mmekuwa mnahadaa wananchi kwa kuita "awamu" wakati chama, viongozi na itikadi ni zilezile. Zama za kudanganyana zimepita
 
Kunywa maji kwanza..!! Rambana Chumvi ushushe Sukari halafu nisome vizuri.

Nyerere aliongelea Uasi! Sifa zikawa kwake
Lissu kaongelea Uasi Kesi imekuja kwake.

Ndio nikasema, kwa watawala kila neno lina maana yake kulingana na mtawala aliyepo.

Bado una Hasira?
 
..halafu Ccm wanajiita chama cha ukombozi kusini mwa afrika.

..lakini harakati za ukombozi zilihusisha matumizi ya silaha kufanya mauaji na kuharibu miundombinu.

..makambi ya frelimo, zanu, zapu, swapo, anc, pac, yalikuwa hapa Tz yalitumika kufundisha makada wa vyama hivyo, kufanya hujuma za kijeshi, na kuharibu miundombinu, ktk nchi zao. Kwa maneno mengine ugaidi.
 
Halafu Wananchi tukitaka kujikomboa tunaitwa Wahaini na Magaidi.
 
Harakati za uMkontho we Sizwe zililenga kulipua na kuharibu miundombinu. Niliwahi kusikia mahojiano ya mtu mmoja wa SA hakutaka kwenda kwenye details ila alisema mafunzo yao walipatia Tanzania.
Halafu Wananchi tukitaka kujikomboa tunaitwa Wahaini na Magaidi.
Wanajishuku. Ukiangalia kwa makini mbinu za kukabiliana na wapinzani ambazo CCM wamezitumia kwa takribani miaka 20 sasa, ni zile zile ambazo tulikuwa tunazipinga na kuzishuhudia zikitumika dhidi ya wanaodai usawa na uhuru wakati wa ukombozi wa Africa hasa kule SA.
 
Haina tofauti na siasa za jukwaan au tambo za mpira au maneno ya mabondia uyapeleke mahakaman
 
Back
Top Bottom