Wapi matajiri wanapatia na maskini wanakosea?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Wakati wote tangu dunia kuwepo, ulimwenguni matajiri ni wachache sana wakati mafukara ni wengi sana. Inakadiriwa asilimia 1 ya matajiri duniani wanamiliki asilimia 50 ya utajiri wote duniani!

Harakati nyingi duniani ni za kuwapa masikini unafu wa maisha. Kuna elimu bure, COVAX, MKUKUTA, LHRC, Amnesty International n.k. Mambo haya yote yanafanyika kwa ajili ya maskini.

Kwanini ni vigumu sana kuwa tajiri kuliko kuwa maskini?

Kwanini pamoja na jitihada nyingi zinazofanywa na maskini au kwa ajili ya mafukara. Bado jamii kubwa ya binadamu imeendelea kubaki katika lindi la umaskini?
 
Utajiri ni discipline ..
Hata wewe ukiwa shule unakumbuka ilivyo ngumu Ku maintain discipline
 
Kufikiri (thinking) hiki ndo kitu kigumu kuliko vyote Duniani.

Anavyofikiri, waza tajiri ni tofauti kabisa na anavyo fikiri, waza maskini
 
Wakati wote tangu dunia kuwepo, ulimwenguni matajiri ni wachache sana wakati mafukara ni wengi sana. Inakadiriwa asilimia 1 ya matajiri duniani wanamiliki asilimia 50 ya utajiri wote duniani!

Harakati nyingi duniani ni za kuwapa masikini unafu wa maisha. Kuna elimu bure, COVAX, MKUKUTA, LHRC, Amnesty International n.k. Mambo haya yote yanafanyika kwa ajili ya maskini.

Kwanini ni vigumu sana kuwa tajiri kuliko kuwa maskini?

Kwanini pamoja na jitihada nyingi zinazofanywa na maskini au kwa ajili ya mafukara. Bado jamii kubwa ya binadamu imeendelea kubaki katika lindi la umaskini?
Mfumo wa Maisha pia Huchangia, Nchi ikiwa ya Kibepari sana kunakuwa na income inequality kubwa.

Nchi za Kiarabu/kiisilamu na Nchi ambazo zina mix ubepari na ujamaa kwa ufanisi zina watu wengi wenye kipato cha kati, masikini kidogo sana na mabilionea kidogo sana.

Mfano Nchi Tajiri za Middle East kama Qatar ama UAE poverty rate ni zero. Hakuna masikini Raia nchi nzima.

Ukija Nchi za Sout East Asia kama Malyasia, Brunei, Singapore etc nao wapo vizuri sana Masikini mpaka chini ya Asilimia 1.

Pia ukienda ukanda wa Scandinavia kama Finland, Norway, Denmark, Sweden nao Pia Wana masikini wa chache. Mfano Norway poverty rate ni 0.5% tu, hio maana yake kila watu 200 mmoja ndio masikini.

Nchi zetu za Ki Africa mambo ni Tofauti Nigeria Wana mafuta Ila yanafaidisha Asilimia 1 tu ya population, mabilionea wengi ila raia wa kawaida wanaishi hovyo, huu ni mfumo wa kibepari.
 
Ukiusoma huo uzi kwenye link hapo chini utaweza kuambulia mawili matatu juu ya mada yako.
 
Anapokosea masikini ndipo hapo hapo tajiri anapopatia, na anapopatia tajiri ndipo hapo hapo masikini anapokosea.
Sijui hata nimesema nini 😂😂😂
 
Utajiri ni discipline ..
Hata wewe ukiwa shule unakumbuka ilivyo ngumu Ku maintain discipline
Hembu fafanua zaidi kuhusu hiyo discipline tuelewe
 
Tatizo hapa unatuuliza masikini. Usitegemee jibu la uhakika. Wenyewe hatujui.
 
Wakati wote tangu dunia kuwepo, ulimwenguni matajiri ni wachache sana wakati mafukara ni wengi sana. Inakadiriwa asilimia 1 ya matajiri duniani wanamiliki asilimia 50 ya utajiri wote duniani!

Harakati nyingi duniani ni za kuwapa masikini unafu wa maisha. Kuna elimu bure, COVAX, MKUKUTA, LHRC, Amnesty International n.k. Mambo haya yote yanafanyika kwa ajili ya maskini.

Kwanini ni vigumu sana kuwa tajiri kuliko kuwa maskini?

Kwanini pamoja na jitihada nyingi zinazofanywa na maskini au kwa ajili ya mafukara. Bado jamii kubwa ya binadamu imeendelea kubaki katika lindi la umaskini?
Kwa sababu umaskini unaanzia kwenye fikra.
Kwa mfano fikiria umeajiriwa na muhindi kumfanyia biashara yake ya restaurant,wateja unawajua,mapishi yote unayajua,lakini miaka yote unabaki kumfanyia kazi muhindi na kuendelea maskini.
Kwa sababu tayari akili yako imeshakariri kuwa wewe umeumbwa ili uwe muajiriwa wa muhindi
 
Back
Top Bottom