Huna haja ya kuanza kutafuta sehemu kama umesoma mpaka chuo,ingawa nakubali kwamba kufika chuo haimanishi mtu yuko vizuri ila naamini una basics na unaweza kujifunza mwenyewe.
Tatizo lako liko na watanzania wengi na chanzo chake ni sisi wenyewe,sijui siku hizi ila wale tuliopita st.Government tulikuwa tunavunjana moyo sisi kwa sisi,watu hawafanyi mazoezi au hawaongei kiingereza muda mwingi,primary na secondary ukiongea english wenzako wanakuona unajiona,unajifanya unajua kumbe in a long run tunaumizana.Kwa level yako nakushauri soma vitabu ukiweza pata vile vya zamani ni vizuri kama "Brighter grammar series, revision English, common mistake in English na vingine vingi.Tafuta watu wa kuongea nao kama una access na mtu anayejua English only it is better,pia angalia movie upime uwezo wako wa kusikia maneno na penda kujisomea vitabu na kusoma habari zilizoandikwa kingereza.Siku hizi resources ni nyingi kuliko unavyoweza kufikiria,youtube unaweza pata video zinazofundisha chochote unachotaka kujua only if you will search using the right words.
Wewe mwenyewe penda kuongea kingereza angalia wazungu wakija Bongo ,muda wote wanataka waongee Kiswahili ,why?Anahitaji kujifunza kutoka kwako.