Wapi naweza kupata fund au sponsorship ya ku-print kitabu changu?

Wapi naweza kupata fund au sponsorship ya ku-print kitabu changu?

Katika biashara isiyolipa Tanzania ni biashara ya vitabu! Watanzania hawana hulka ya kujisomea labda uende Chuo Kikuu cha Dar walazimishe kiwekwe kwenye mitaala. Vinginevyo kiwe e-book mtandaoni waki download Amazon upate fedha zako!
Hata hizo e book wanataka za bure Kwa kifupi wabongo na shortcut ni damu Damu
 
Katika biashara isiyolipa Tanzania ni biashara ya vitabu! Watanzania hawana hulka ya kujisomea labda uende Chuo Kikuu cha Dar walazimishe kiwekwe kwenye mitaala. Vinginevyo kiwe e-book mtandaoni waki download Amazon upate fedha zako!
Mkuu mimi wateja wangu ni watoto na wanunuzi sijalenga sana individuals kuna taasisi nafikiria kuwauzia wao wanunulie watoto. Ipo kitofauti kidogo. Ila pia nafikiria kuuza online kama Amazon.
 
Una authority behind ya unachokiandika au kwenye auandishi, mfano Diamond akiandika kitabu kuhusu mziki kitanunulika tu au Mkapa na Reg Mengiwalikuwa na authoy behind je wewe hauna authority wala audience unawezaje kuuza
Ulichokisema ni kweli. Mimi ni mwandishi pia wa novels, kazi ya uandishi ni ngumu kuliko anavodhani
 
Kama financial education why usiitumke iyo elimu ili upate pesa ama unajua tu kuongea sema practical zero?
The talk is the cheapest that can be performed by anyone...
Siandiki motivational books mkuu. Nafundisha watoto kuhusu pesa ni kama maarifa ya jamii, hesabu, ICT nk
 
JF umekuwa mtandao wa hovyo wa kuwakatisha watu tamaa na kuharibu mijadala ya kujenga jamii. Hapa umeleta wazo zuri lakini kwa baadhi ya watu hovyo kabisa!
Mkuu awa wakatishaji tamaa mimi siwazingatii kabisa ndio maana nawajibu wanachostahiki. Watu wenye kukujenga hata wakijitokeza wawili wanatosha sana.
 
Nenda kwa wahusika yaani taasisi za wanawake na wadau wao. Yaani uandike vitabu ambavyo ndio matokeo ya kutuletea changamoto kwenye mahusiano halafu sisi tukuchangie pesa?
Pole mkuu kwa changamoto za kimahusiano zinazokusumbua. Nashauri tu ukiwa kwenye mahusiano simama kama mwanaume utakuwa kichwa kwenye relationship yako. Pia mimi sijaomba unichangie hela au comprehension ni tatizo?
 
Ungeandika vitabu vyenye Title kama hizi ungeuza sana
"UTAMU WA TUNDA NI KUPEANA "
"UCHAWI SASA BASI NIMEKOMA"
"NILIVYO TOROKA KUZIMU"
Hao ndio watanzania, hivyo ndio vitabu vyao.
ANaweza tokea mtu akadhamini lakini, endelea kukaza.
 
Sema mtoa post anaonekana jeuri sana ukiangalia lugha yake....
Hii ndio shida. Uwezo wa kumsaidia ninao na hata kumkutanisha na wadau. Ila hata maswali ya kawaida tu anapanick. Asipochukua ushauri wako basi tena. .
 
Mtindo wa decoding ndiyo mtindo gani mkuu?
Ni hadithi zinazozingatia kufundisha vitu vingi kwa wakati mmoja ikiwemo herufi sauti silabi na maths na elimu nyingine utayochagua mtunzi. Rajabu anafanya hesabu huku anatafuna zabibu.
 
Hii ndio shida. Uwezo wa kumsaidia ninao na hata kumkutanisha na wadau. Ila hata maswali ya kawaida tu anapanick. Asipochukua ushauri wako basi tena. .
Nasisitiza sihitaji msaada wako mkuu.
 
Back
Top Bottom