Wapi naweza kupata 'hearing aid device' kwa bei rahisi?

Wapi naweza kupata 'hearing aid device' kwa bei rahisi?

Mimi pia nina hiyo shida nilinunua hapo Hearwell mwaka 2014 ,kwa bei karibia na uliyosema, nikatumia nikaona vinanikera nikaamua kuachana navyo,

Nenda buguruni malapa shule ya Viziwi kuna wazungu huwa wanakuja kila mwaka kufanya vipimo vya masikio na kutoa hearing Aid bure baada ya vipimo, nenda ukaulize ratiba zao huwa zikoje, wanakuja mwezi gani.

Lakini pia kwa ushauri wangu, inabidi kwanza ujikubali na hali mpya, hearing Aid quality ya sauti haifanani na quality ya sauti ya sikio lisilo na tatizo, zingine zinaumiza masikio, zinaweza zikaharakisha uziwi.
Hearing Aid Devices Zina Faida na hasara zake shida kubwa ya vile vifaa ni wepesi wa kunasa sauti hata zisizo na maana,

Unapotumia hizo mashine utulivu kichwani huondoka, kichwa huuma na mwili huchoka.

Eneo la nje la sikio huvilia Damu maana unapovaa kile kifaa huziba tundu lote la sikio na hivyo huzuia hewa kuingia sikioni, mgandamizo wa joto hupelekea sikio kuwasha kwa ndani.

Kimsingi Faida ya hivyo vifaa ni ndogo kuliko madhara yake, Kadri unavyoendelea kuvitumia hali ya usikivu wako wa asili huendelea kupungua.

Suluhisho rahisi kwa wote wenye hali hii ya usikivu hafifu hakikisha kwamba unajikubali jinsi ulivyo na unaifurahia hali yako.

Kuhusu dawa kuna dawa nzuri inayosaidia kuzibua mishipa ya sikio ni m,badala mzuri wa hiyo Neuro Support ambayo ni Combination ya Vitamin B1,B6, B12 na Folic Acid.

Hiyo dawa jina limenitoka ila ni nzuri sana ndo maana nashauri muungane kwa kuwa na hata group moja litakalowasaidia kushare vitu tofauti.

Ni vyema pia kuzingatia usafi wa sikio Kila uamkapo na kabla ya kulala, hakikisha Kila baada ya muda Fulani kupitia unaenda kuzibua sikio maana mengine huwa yanajaa maji na vumbi.

Naelewa ni kwa kiasi gani hii hali huwakwaza sometimes but kitu kikubwa ni kujikubali, kuielewa hali yako na kuweza kuicontrol.

NB: Unapokuwa na mapungufu Fulani ya kimwili ama ulemavu hakikisha status yako ipo juu siku zote kama kusoma soma kweli kweli, kama una kazi fanya kazi 200% ili kucover mapungufu yako kuepuka watu kukupuuza na kukudharau. Kamwe usipende kutumia hali yako kama ngazi ya kutaka uhurumiwe au upendelewe.
 
achana navyo havina msaada njoo tukufundishe lugha za Alana uongee Kama wasiosikia.

hizo hearing aids kazi yake ni kukushtua endapo kutakuwa na kitu kimedondoka kwa suti kubwa havina uwezonwa kukutafisiria maneno.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Kuna taasisi inaitwa Starkey Hearing Foundation huwa wanakujaga Tanzania hupima na kutoa devices bure kwa Makundi ya watu tofauti .

Ni taasisi iliyoenea ulimwenguni na huja Mara moja kwa mwaka. Wenye uhitaji wa mawasiliano nao naweza kuwalink
 
Back
Top Bottom