Wapi naweza kupata idadi ya Tarafa nchini

Abuu hanifa

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2021
Posts
256
Reaction score
275
Nina swali dogo hili.

Hivi mfumo wa serikali unatambua uwepo wa tarafa?

Nahitaji kupata orodha ya tarafa zote nchini, wapi naweza kupata link au document hiyo?
 
Nina swali dogo hili. Hivi mfumo wa serikali unatambua uwepo wa tarafa? Nahitaji kupata orodha ya tarafa zote nchini, wapi naweza kupata link au document hiyo?
... kwa mujibu wa TAMISEMI, jumla ya tarafa nchini ni 570 (Hisoria ya Taasisi | PO-RALG) ila kwa kuwa unahitaji orodha jina kwa jina jaribu kufika ofisini kwao.
 
... kwa mujibu wa TAMISEMI, jumla ya tarafa nchini ni 570 (Hisoria ya Taasisi | PO-RALG) ila kwa kuwa unahitaji orodha jina kwa jina jaribu kufika ofisini kwao.
Mbona katika nyaraka nyingi za serikali kinachoonekana ni mkoa (region) wilaya (district), kata (ward), kijiji (village), mtaa (street) na kitongoji (hamlet, subvillage, suburb ) pekee?
 
Mbona katika nyaraka nyingi za serikali kinachoonekana ni mkoa (region) wilaya (district), kata (ward), kijiji (village), mtaa (street) na kitongoji (hamlet, subvillage, suburb ) pekee?
Kwa kweli hata mimi sijui kwanini tarafa/divisions hazihusiki sana kiserikali. Labda ni kupunguza mzigo wa uendeshaji.
 
Wakitoka kata wanaruka mpaka wilaya, Tarafa ni muundo wa zamani ndomaana hazina nguvu kwa sasa ila kimuundo inakuwa kati ya wilaya na kata... kuna klasta pia sijui mliwahi kuisikia hii nayo?
 
Wakitoka kata wanaruka mpaka wilaya, Tarafa ni muundo wa zamani ndomaana hazina nguvu kwa sasa ila kimuundo inakuwa kati ya wilaya na kata... kuna klasta pia sijui mliwahi kuisikia hii nayo?
Precisely badala ya wilaya ita halmashauri ambazo kwa kawaida huundwa na mabaraza ya madiwani ambao hutokea kata na sio tarafa.
 
Sina hakika kama kwa sasa tarafa zina watendaji; labda kwa muundo wa zamani.
Miji midogo ambayo bado kupandishwa hadhi ku wilaya ina viongozi hawa.

[d] Ngazi ya Tarafa Kwa mujibu wa muundo Mamlaka za Miji) Sura ya 288 inaelekeza kwamba Wilaya itagawanywa katika Tarafa ili kuwa kiungo kati ya Serikali Kuu, Halmashauri na Ngazi ya Kata. Mji Mdogo hutambulika kama Mamlaka ya Mji Mdogo. Mamlaka ya Mji Mdogo ni Mamlaka ya Serikali za Mitaa iliyopo katika mamlaka za Wilaya na ambayo imeanza kuendelezwa na kuwa na mazingira ya kimji. Kimsingi mamlaka ya mji mdogo hutokana na eneo la Kijiji au Vijiji vilivyoanza kuonyesha dalili za kuendelezwa na kuwa na mazingira ya kimji. Mamlaka hii huanzishwa baada ya kutimiza vigezo maalum ambavyo ni pamoja na kuwa na wakazi wasiopungua 10,000, kuwa na eneo lenye kilomita mraba 580, huduma za msingi za kijamii kama vile shule, vituo vya afya, maji na barabara kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa Kitaifa kwa kila sekta husika. Muundo wa mamlaka hizo kwa mujibu wa sura 287 ya sheria, hujumuisha wajumbe wafuatao:- - Mwenyekiti ambaye atachaguliwa miongoni mwa Wenyeviti wa Vitongoji; - Wenyeviti wa Vitongoji vilivyomo katika eneo la Mamlaka; - Wajumbe walioteuliwa na Halmashauri ya Wilaya wasiozidi watatu; - Mbunge anayewakilisha jimbo ambamo Mamlaka hiyo imo; - Wajumbe viti maalum ambao hawatapungua robo ya wajumbe waliotajwa hapo juu. - Katibu wa Mamlaka ya Mji Mdogo ambaye ni Afisa Mtendaji wa Mji Mdogo, lakini hatakuwa na sifa ya kupiga kura. Utendaji wa Mamlaka ya Mji Mdogo huwezeshwa kupitia kamati za kudumu zifuatazo:- - Kamati ya Kudumu ya Fedha, Utawala na Mipango Miji; - Kamati ya Kudumu ya Elimu, Afya na Maji; - Kamati ya Kudumu ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira.
 
Shukran kwa nondo hizi muhimu.

Kwa kuongezea juu ya suala la tarafa kadiri nijuavyo.

Mtiririko uko hivi.

Upande wa Usimamizi wa Serikali
Rais
Mkuu wa mkoa
Mkuu wa wilaya
Katibu tarafa.

Kwa upande wa utendaji
Waziri mkuu
Mkurugenzi wa halmashauri
Watendaji wa kata
Wenyeviti wa serikali za mitaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…