Miji midogo ambayo bado kupandishwa hadhi ku wilaya ina viongozi hawa.
[d] Ngazi ya Tarafa Kwa mujibu wa muundo Mamlaka za Miji) Sura ya 288 inaelekeza kwamba Wilaya itagawanywa katika Tarafa ili kuwa kiungo kati ya Serikali Kuu, Halmashauri na Ngazi ya Kata. Mji Mdogo hutambulika kama Mamlaka ya Mji Mdogo. Mamlaka ya Mji Mdogo ni Mamlaka ya Serikali za Mitaa iliyopo katika mamlaka za Wilaya na ambayo imeanza kuendelezwa na kuwa na mazingira ya kimji. Kimsingi mamlaka ya mji mdogo hutokana na eneo la Kijiji au Vijiji vilivyoanza kuonyesha dalili za kuendelezwa na kuwa na mazingira ya kimji. Mamlaka hii huanzishwa baada ya kutimiza vigezo maalum ambavyo ni pamoja na kuwa na wakazi wasiopungua 10,000, kuwa na eneo lenye kilomita mraba 580, huduma za msingi za kijamii kama vile shule, vituo vya afya, maji na barabara kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa Kitaifa kwa kila sekta husika. Muundo wa mamlaka hizo kwa mujibu wa sura 287 ya sheria, hujumuisha wajumbe wafuatao:- - Mwenyekiti ambaye atachaguliwa miongoni mwa Wenyeviti wa Vitongoji; - Wenyeviti wa Vitongoji vilivyomo katika eneo la Mamlaka; - Wajumbe walioteuliwa na Halmashauri ya Wilaya wasiozidi watatu; - Mbunge anayewakilisha jimbo ambamo Mamlaka hiyo imo; - Wajumbe viti maalum ambao hawatapungua robo ya wajumbe waliotajwa hapo juu. - Katibu wa Mamlaka ya Mji Mdogo ambaye ni Afisa Mtendaji wa Mji Mdogo, lakini hatakuwa na sifa ya kupiga kura. Utendaji wa Mamlaka ya Mji Mdogo huwezeshwa kupitia kamati za kudumu zifuatazo:- - Kamati ya Kudumu ya Fedha, Utawala na Mipango Miji; - Kamati ya Kudumu ya Elimu, Afya na Maji; - Kamati ya Kudumu ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira.