Scaboma
JF-Expert Member
- Jul 29, 2018
- 335
- 212
Habari za majukumu wadau,
Mie ni mjasiriamali mdogo wa nafaka, natoa mikoani nazileta mjini nauza kwa jumla, Sina fremu ya kufikishia biashara yangu hivyo nikifika madalali hunidaka na kunidalalia kwa wanaouza kwa jumla nami nageuza zangu shamba. Hii hali nimejikuta kama nawatajirisha madalali waliokaa mjini na kunisubiria wanipangie bei, hivyo nimeona ni bora niwe na fremu zangu za kufikishia mzigo ili niwe nauza taratibu kwa bei nzuri, tatizo linakuja mtaji wangu bado mdogo, nikiziipia fremu nitapunguza mtaji.
Naomba mwenye kujua sehemu nayoweza kupata mkopo wa masharti nafuu, nimejaribu kwenye mabenki na baadhi ya microfinance wanahitaji niwe na fremu ya kuuzia biashara yangu pamoja na mlolongo wa business documents, kitu ambacho kwa Sasa Sina ila nikipangasha fremu lazima nikatie documents zote.
Nina shida ya 10M ili niweze kuboresha biashara yangu iendane na wakati, dhamana yangu ni nyumba ipo Mbezi Beach ina hati ya serikali ya mtaa, naomba mwenye kufahamu sehemu nayoweza kupata mkopo wa masharti nafuu tofauti na bank tujuzane tafadhali.