Wapi naweza pata wafanyabiashara wa bidhaa hizi ambao wako tayari kuuza bidhaa zao kwa wingi zaidi ila kwa mkopo wa muda mfupi?

Mimi siwi wakala mkuu. Utanidai wateja kwa kadri ya uwezo wako na pesa za mauzo
Hii itategemea mzigo utachukua siku ngapi kuisha. Kama utachukua siku chache mfano siku 3 stock ya mifuko 500 ya simenti kuisha unaweza kumvutia au kumshawishi mzalishaji, huku akijua ndani ya siku 3 anapata fedha zake. Kazi kubwa uliyonayo, ni kumhakikishia mzalishaji kuwa una wateja wakutosha na ndani ya muda mfupi mzigo utakuwa umeisha; tofauti na hapo biashara itakuwa ngumu.

Pia ili kujiweka smart na kuaminika kibiashara, ni vizuri ukasajili kampuni, mfano xxxxx general traders n.k baada ya hapo tembelea viwanda unavyovifahamu uwashawishi ili muingie makubaliano ya hiyo biashara yako unayotaka kufanya.
 

Utasema wewe uko wapi, mimi nitaangalia market share ya hiyo wilaya au mkoa. Ila mifuko 500 ya cement ni michache kwa siku3 kwa jinsi nilivyogawa masoko. Naomba nikuweke kwenye list yangu kabisa tupunguziane stress ya pesa na kazi🤣🤣🤣🤣

Asante kwa ushauri kakake mimi
 
Nadhani wapo wengi tu, ila wengi wao wanataka kwanza down payment (yaani kama unataka mzigo wa 10m wanata utoe 5m ama 6m kwanza) ndipo zingine ulipe polepole. Wengineo wanataka uwe umefanya nao biashara kwa muda kidogo kabla hawajaanza kukukopesha, ili wajue kwanza mzunguko wa biashara yako. Ni hayo yo Mama D
 
Asante sana Idimi 🙏
Tunaweza kuongea na kuona mkataba uwe vipi, kwa faida ya pande zote.
 
Asante sana Idimi 🙏
Tunaweza kuongea na kuona mkataba uwe vipi, kwa faida ya pande zote.
Nadhani wahusika watakuja inbox, mie nilitoa mtazamo wangu kwa kadri ya uzoefu wangu mdogo sana kwenye biashara.
 
NIPIGIE 0785515762 NIKUSAIDIE UPATE INSURANCE BOND PIA NAWEZA KUKUSAIDIA KUKUUNGANISHA NA BAADHI YA VIWANDA VYA BUILDING MATERIAL AMBAO TUNAFANYA NAO KAZI KWA WAO KUTOA CRETIDTY FACILITY KWA WATEJA WAO SISI TUNATOA INSURANCE BOND
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…