Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sina uzoefu na dawa ya kuzuia magugu kuota ila nina uzoefu na dawa ya kuua wadudu. Inamaana kama utazuia kuota magugu automatically hata mimea yako ambayo umepanda haitaota vizuri au haitaota kidogo. Tafuta dawa za kupalilia kutoka kwenye maduka ya pembejeo. Kama vipi chukua hilo jani likiwa bichi nenda nalo kwa duka la pembejeo muonyeshe then mueleze tatizo lako. Au kama vipi muone mtaalamu wa kilimo aliye karibu nawe. Siku hizi kuna mabwanashamba wa kata na vijiji.Wadau, natafuta kwa udi na uvumba kama kuna dawa ya kuzuia magugu yasiote. Yananisumbua sana, kila siku yanaoteana tu. Nipo Dar es Salaam.
Natanguliza shukrani.
Sina uzoefu na dawa ya kuzuia magugu kuota ila nina uzoefu na dawa ya kuua wadudu. Inamaana kama utazuia kuota magugu automatically hata mimea yako ambayo umepanda haitaota vizuri au haitaota kidogo. Tafuta dawa za kupalilia kutoka kwenye maduka ya pembejeo. Kama vipi chukua hilo jani likiwa bichi nenda nalo kwa duka la pembejeo muonyeshe then mueleze tatizo lako. Au kama vipi muone mtaalamu wa kilimo aliye karibu nawe. Siku hizi kuna mabwanashamba wa kata na vijiji.
Okay. Basi tumia dawa ambayo ni non selective kwa magugu. Nakushauri ukifika Agrovet ulizia roundup dawa ya kuua magugu. Pia kama huna haraka na hilo shamba, fanya kitu kinaitwa weed timing control. Yaache yaote yote kwanza halafu yakishatoa maua ndo uyadhibiti either kwa kulima au kutumia dawa. Usikubali yatoe mbegu ili kuzuia kuenea zaidi. Yakitoa tu mbegu hutaweza kuya control maana dispersal itakuwa kubwa sana. Ndo namna tunavyodili na magugu hasa noxious weed ambayo ni magumu kuzuia. Ila dawa nzuri ni round up.Shukrani. Magugu haya yanajiotea tu kila sehemu. Haipiti wiki inabidi kuyang'oa. Inabidi kuchukua hatua. Kama kuna dawa ya kuua wadudu unaona itafaa naomba unijulishe, hakuna mimea mingine itakatoathirika.
Nchi kavu. Ni mazingira ya nyumbani.
Mimi kuna dawa natumia sana kwa ajili ya kilimo cha mpunga inaitwa Tiller gold lakini inabagua magugu ila wewe ningekushauri uende duka la pembejeo za kilimo ukawaambie aina ya majani yanayokusumbua watakupa sumu Nb: sio majani yote yatakauka labda upige bomu la nuclear hapo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Okay. Basi tumia dawa ambayo ni non selective kwa magugu. Nakushauri ukifika Agrovet ulizia roundup dawa ya kuua magugu. Pia kama huna haraka na hilo shamba, fanya kitu kinaitwa weed timing control. Yaache yaote yote kwanza halafu yakishatoa maua ndo uyadhibiti either kwa kulima au kutumia dawa. Usikubali yatoe mbegu ili kuzuia kuenea zaidi. Yakitoa tu mbegu hutaweza kuya control maana dispersal itakuwa kubwa sana. Ndo namna tunavyodili na magugu hasa noxious weed ambayo ni magumu kuzuia. Ila dawa nzuri ni round up.