Wapi nitapata mashuka ya mtumba ya kulenga

Wapi nitapata mashuka ya mtumba ya kulenga

Apo Tandika sokoni Mashuka ni muda wote au natakiwa kudamka allfajili. Pia vip kuhusu bei zao maana lengo ni kununua na kwenda kuuza.
Kuhusu ratiba sahihi na muda sina hakika ila ukifika pale asubuhi ni vyema kama utakuwa na nia kubwa ya kutaka kujua, at least saa 1 au 2 sio mbaya. Utakuta mnada wa mashuka na bed covers za kutosha. Na bei last time nilikuta ni 4k,6k na 8k.. zinacheza kulingana na ubora wa shuka na size. Nikutoe hofu Tu ndugu pale mashuka ni bei rahisi na ni mazuri Sana na pia pengine hata yasifike hiyo 8k ila ni vyema ukabeba pesa yakutosha ili upate mziko mwingi na mzuri.

Kama nitapata info zaidi nitajazia maana sijapita pale kitambo kidogo. Kumbuka pia location ni TANDIKA SOKONI.

ASANTE.
 
Nimejaribu kuuliza zaidi nimejuzwa kuwa mnada unafanyika siku za wiki mida ya saa 3 asubuhi na mara chache saa 4. Kuhusu location na mengine nliyoeleza hapo juu yanabaki the same.🤝
 
Nina mtaji wa laki na nusu, naomba kujuzwa wapi wanauza mashuka ya mtumba kwa bei rahisi ninunue kwa lengo la kuja kuuza mtaani kwetu.
Kama unauza jifunze na wewe kununua anaponunua muuzaji, huyo wa Tandika kuna sehemu ananunua Belo na yeye anakuja kumwaga anakuuzia wewe.

Ukichukua Belo lako hapo kwa mtumba roughly ni 1000 haijalishi ni Shuka, Gauni etc.

Mfano kama hivi

View: https://www.instagram.com/businesseaglesstartup/reel/Cyp2gVRtTb6/

Sema kuwa makini usimpe mtu hela bila kupewa Mzigo physically.
 
Back
Top Bottom