Wapi nitapata Mbwa wa kufuga?

Wapi nitapata Mbwa wa kufuga?

Kashaija

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2008
Posts
255
Reaction score
62
Tafadhali kwa anayejua mahali ninakoweza kupata Mbegu nzuri ya Mbwa anifahamishe.

Namuhitaji sana hata kama nikipata wawili maana vibaka wananikera sana nyumbani kwangu, ila asiwe Mbwa koko.
 
Mkuu kama upo Dar ukitembelea barabara ya Ali Hassan Mwinyi maeneo ya kuanzia Victoria kuelekea Morroco, nawaonaga vijana wanasimama pembezoni mwa barabara kuuza vi-jibwa na ma-mbwa, unaweza kuchungulia ukipata muda ukaona variety na bei zao.
 
In the meantime fortunately I am in Tanzania and I will be selling my German shepherd puppies for US$ 500.00 each. Send me an email and we can start from here!
 
Tafadhali kwa anayejua mahali ninakoweza kupata Mbegu nzuri ya Mbwa anifahamishe.

Namuhitaji sana hata kama nikipata wawili maana vibaka wananikera sana nyumbani kwangu, ila asiwe Mbwa koko.

Kama upo dar jioni katiza barabara ya new bagamoyo maeneo ya victoria kuna jamaa wanauza breed tofauti tofauti.Pole sana na vibaka ila kuwa makini na hao mbwa kuna hatari nyingine ya kupata kesi kama hadithi ya juzi huko mbezi beach. Nakushauri weka walinzi wa makampuni binafsi tena wakikufungia na security alarms zao gharama si kubwa kama kufuga jibwa moja.
 
Mkuu kama upo Dar ukitembelea barabara ya Ali Hassan Mwinyi maeneo ya kuanzia Victoria kuelekea Morroco, nawaonaga vijana wanasimama pembezoni mwa barabara kuuza vi-jibwa na ma-mbwa, unaweza kuchungulia ukipata muda ukaona variety na bei zao.

Thanx, nitajaribu kupitapita, ila nadhani zoezi lenyewe ni la kubahatisha bahatisha, wangekuwa na specific day au kama wangekuwa na contacts ingekuwa bora zaidi.
 
Thanx, nitajaribu kupitapita, ila nadhani zoezi lenyewe ni la kubahatisha bahatisha, wangekuwa na specific day au kama wangekuwa na contacts ingekuwa bora zaidi.

Kweli hilo ni tatizo mkuu.
 
Nenda Iringa mazee unaweza pata hata Fuso lililojaa Mbwa! I am not joking.....Iringa kuna mbwa wengi kuliko idadi ya wakazi wa huko!
 
In the meantime fortunately I am in Tanzania and I will be selling my German shepherd puppies for US$ 500.00 each. Send me an email and we can start from here!

Mshiiri,

Are you really serious? US$ 500.00 per each? what is so special with German shephead puppies/dog?
 
Thanx, nitajaribu kupitapita, ila nadhani zoezi lenyewe ni la kubahatisha bahatisha, wangekuwa na specific day au kama wangekuwa na contacts ingekuwa bora zaidi.

Sasa wewe si muhitaji...Wale hawana siku wala muda wapo kila siku na kila wakati, hawabahatishi....... ukifika victoria usipowaona ulizia utaitiwa...
 
Mshiiri,

Are you really serious? US$ 500.00 per each? what is so special with German shephead puppies/dog?

mkuu hiyo ni bei sawia kwa breed hii, lakini pia inategemea na umri wao.
pale shoperz plaza mlango wa kuingilia supermarket kuna matangazo mengi tu ya wanaouza mbwa,jaribu kupita pale! mimi nilichukua namba na nikampigia mhusika mmoja akadai yuko kijitonyama na anauza puppies wa germany shepherd kwa 400,000, ninaweza kukupatia contact kesho kama utashindwa kupitia. Hii ni breed nzuri kwani wanafundishika kirahisi mno na wana nidhamu na wako friendly kwa watoto tofauti na koko.
otherwise nina germany shepherd nimemfanyia cross breed na rottweiler atazaa mwezi wa sita mwishoni unaweza fanya booking kama bado utakuwa hujapata
 
Nenda Iringa mazee unaweza pata hata Fuso lililojaa Mbwa! I am not joking.....Iringa kuna mbwa wengi kuliko idadi ya wakazi wa huko!

aaah wapi, washaliwa supu wote! ....tehteehh (joke)
 
Tafadhali kwa anayejua mahali ninakoweza kupata Mbegu nzuri ya Mbwa anifahamishe.

Namuhitaji sana hata kama nikipata wawili maana vibaka wananikera sana nyumbani kwangu, ila asiwe Mbwa koko.

Piga simu namba 0754813440. Kama wapo. Bei shs 200,000-300,000. Utafurahia.
 
"Nenda Iringa mazee unaweza pata hata Fuso lililojaa Mbwa! I am not joking.....Iringa kuna mbwa wengi kuliko idadi ya wakazi wa huko!"
Ndio jambo Forum. Lakini nakukatalia kwa sababu kule awe German...au koko wote matumizi yao ni mamoja,haiwezekani kabisa wakawa wengi zaidi.
 
Mazee nenda pale police dog section wape dili wale jamaa wanaweza kukufanyia mpango ukapata wakali kama wa mzee
 
Usishangae mkuu $500 kwahiyo kitu ni sawa bin sawia kabisa, ni mbwa wazuri sana na utawa treat unavyotaka, wana heshima na ni walinzi wa ukweli
Otherwise makoko nao wapo wengi tu tena bure, ukisikia mbwa wa jirani kazaa unaomba anakupatia vitoto viwili buree, kimoja kinakua kingine kinakufa unasonga mbele na hicho kinachokua baada ya miezi kadhaa zinaanza kesi za kula kuku wa watu mtaani unamfungia siku ukijisahau akatoka anaona isiwe tabu anachapa zake mwendo mtaani anaishia jumla unamwambia tena jirani akupe kitoto kingine.....
 
KAMA HUYU.?

[ame=http://www.youtube.com/watch?v=37gZHVr5slo]YouTube - Corgi Dog Barks Jingle Bells[/ame]
 
Dawa ya vibaka sio mbwa.Mtafute babu mmoja mwenye haiba ya kiustaadh,aje na vijana wawili watatu...wafanye kisomO hata kama ni cha kisanii,ubani na udi kwa wingi...salamu zitafika.Ukitaka kumtisha mwafrika usimletee habari za sheria,chombo cha dola au mbwa,MWAMBIE UTAROGWA!
 
Back
Top Bottom