Wapi nitapata mtaalam wa tiba ya tezi dume?

Naomba kufahamu ni hospital gani au Dr gani anaweza saidia tiba ya tezi dume.

Mzee wangu ameonekana na tezi dume kwa vipimo vya awali.

Mgonjwa yupo Morogoro.
huku tarime wanaita ugonjwa wa wazee, hii kitu inaongezeka kwa kasi
sisi huku tunakimbilia kisii
ila kwa dar nishasikia mtu ametibiwa kairuki
 
"Akizungumzia matibabu ya ugonjwa huo Dkt. Isaka amesema inategemea na ukubwa wa tatizo ambapo katika hatua za awali mgonjwa anaweza kutumia dawa na tatizo kupona kupona kabisa.

Aidha, kama Mgonjwa atachelewa kupata matibabu katika hatua za awali atalazimika kufanyiwa upasuaji wa kawaida na kutoa tezi au kufanya upasuaji kwa kutumia vifaa maalum (minially invasive procedure).

Dkt. Isaka pia ameitaka jamii kutumia dawa kwa usahihi, kufuata maelekezo ya daktari ambapo itamfanya arejee katika hali ya kwaida na kuendelea na shughuli zake baada ya wiki sita hadi nane.

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila inatoa huduma za uchunguzi na matibabu ya tezi dume, kwa ushauri zaidi fika hospitalini katika kliniki ya Magonjwa ya Mfumo wa Mkojo kila siku ya Jumanne na Alhamisi kuanzia saa 2:00 Asubuhi-9:00 Alasiri, Ghorofa ya kwanza."

Mwisho wa kunukuu.
 
Muhimbili nitaanzia kujaribu hapo maana private bima wanasumbua.
Mloganzila mzee hawezi kukubali kutokana na hearsays mitaani.
 
Nakutumia namba,tezi dume inatibika bila upasuji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…