Wapi nitapata pump ya maji inayotumia diesel/ petrol

M-pesa

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2011
Posts
602
Reaction score
152
Nimechimba kisima cha kawaida, sasa natafuta pump ya kuvuta maji umbali wa mita 60 na kupandisha juu yatumike kwenye imwagiliaji. Sihitaji pump ya kuzamisha ndani ya kisima, nahitaji pump ambayo ni portable.
Asanteni
 
M-pesa

umechimba open pit au borehole?

umechimba na mashine au nguvu kazi?

na kama ni bore hole umeshazamisha casing pipes?

makadirio ya ujazo wa maji utakayotumia na uwezo wa reservior/storage tanks zako ukoje?
 
Nimechimba open pit mkuu! Nimewatumia vijana. Nategemea kununua tenki la litres 5000 tu mkuu. Je, unaweza kunielekeza aina ya pump pamoja na sehemu nitakayoipata? Asante

mkuu kuvuta maji kutoka 60 meters siyo mchezo,kwanza kuchimba open pit mita 60 ni shughuli ndefu,au unamaanisha unasukuma maji kwenda mita 60.
kwa maji kutoka kina cha mita 60 utahitaji submersible pump. nenda Davis & Shirtliff wapo DAR ,victoria na pale kamata ,hawa jamaa wana pump za kijerumani bei yao iko juu,ila ukichukua ni mkataba

kwa maji kutoka open pit kina kifupi kwenda mita 60 ,mimi nilishawahi kutumia a cheaper option
generator ndogo plus pump za pedrolo ya 1hp inatosha kufanya kazi ya kujaza lita elfu 5.
au nunua submersible pump za kichina,Doing etc na generator ndogo ya diesel ,lita elfu 5 utajaza ndani ya saa1
bei ya generator nzuri ni around laki 9
pump ni around laki 4 (mchina)
so tarajia kutumia 1.3 mil
 
nashukuru mkuu, nitawatembelea hawa jamaa wa davis and shirtliff.

Kaka hawa vijana umewapata wapi? Na umewalipaje? Natafuta nguvu kazi na mimi nitoboe mwamba. Walitumia siku ngapi? Kambi aliifadhili nani?
 
Nilimtumia mzee mmoja na vijana wake wawili! Walitumia wiki moja tu maji yakawa yamepatikana. Bei ni laki tano na nusu, lakini mifuko ya cement ambayo inatumika kutengenezea rings zinazozamishwa kisimani ilikuwa juu yangu.
Kambi sikugharamia kwa sababu huyo mzee na vijana wake wanatokea maeneo jirani na shamba langu. Ukihitaji contacts zake tafadhali pm nikurushie.

Kisima cha mita 60 waone Davis & Shirtliff wanayo pump ya sola inavuta na kusukuma maji vizuri sana, wanauza shilingi milioni tano.
 
Hiyo bei mkuu ni kubwa mno, inabidi nijipange.

Shukran sana. Haipishani sana na ninaowafahamu mimi, wao ni 1.6m lakini wanakijengea kabisa, na pump wanaweka, kwahiyo 5.5k + 9k (ya pump) ni 14.5 na mifuko ya cement nk, wako fair. Ntaendelea tu na hao wangu, kwani nimeshawapeleka shamba wakaona na tumeshakubaliana, ila kama bei yako na yao ingekuwa tofauti sana ningewatosa.

Shukran tena na tena.

Nb: kuna mtu mmoja aliwahi kuniambia hapo baadae tz itakuja kusumbuliwa na matetemeko kwasababu idadi ya watoboa miamba (wachimba visima) inakua kwa kasi sana. Hapo vipi wakuu?
 
unataka zile kama kuna mafuriko zinanyonya maji ama pump zipi hizo?
 
Kisima cha mita 60 waone Davis & Shirtliff wanayo pump ya sola inavuta na kusukuma maji vizuri sana, wanauza shilingi milioni tano.
kisima kachimba kwa chini ya mil 2, pump million 5 - hapo kazi ipo
 
Pump za sola, gharama ya manunuzi ni kubwa, gharama za uendeshaji ni sufuri, kulinganisha na pump ya dizeli unanunua kwa gharama ya chini ya shilingi 500,000/= lakini kila siku inapowashwa kuna gharama za kufuata mafuta kwenye vituo na kuyanunua kwa bei elekezi au kwa bei ya kuruka hasa maeneo mengi ya vijijini.
 
Ohoooo sasa nyinyi mtatuletea irani na uturuki haya mambo ya matetemeko tena mimi toka nijue dunia huwa nayaona kwenye luninga tu jamani kama ndo hivyo nawaomba hiyo nshu yakuchimba ipotezeeni mbona hii hali tunayo sikunyingi bilamaji tunaishi ndio MAISHA BORA KWA MTZ

Nb: kuna mtu mmoja aliwahi kuniambia hapo baadae tz itakuja kusumbuliwa na matetemeko kwasababu idadi ya watoboa miamba (wachimba visima) inakua kwa kasi sana. Hapo vipi wakuu?[/QUOTE]
 
Pump za sola, gharama ya manunuzi ni kubwa, gharama za uendeshaji ni sufuri, kulinganisha na pump ya dizeli unanunua kwa gharama ya chini ya shilingi 500,000/= lakini kila siku inapowashwa kuna gharama za kufuata mafuta kwenye vituo na kuyanunua kwa bei elekezi au kwa bei ya kuruka hasa maeneo mengi ya vijijini.

but at least pump ya generator ina zungusha pesa, yaani unatoa pesa kidogo kidogo na unazlisha, unauza then unanunua mafuta then unazalisha, unauza mazao there you go.
 
We are on the same page mkuu! Hata mi sipo tayari kuifunga pesa yangu nyingi kwenye pump. Nitakwenda taratibu mpaka niwe assured kwamba project ina ROI kubwa ya kueleweka.
but at least pump ya generator ina zungusha pesa, yaani unatoa pesa kidogo kidogo na unazlisha, unauza then unanunua mafuta then unazalisha, unauza mazao there you go.
 
heri nyie mnazungumza mambo ya maana,siyo kila siku lema lema lema lema lema lema and...............lema,mtu mwenyewe jambazi!
 
Back
Top Bottom