wapi ntakopa bila salary slip?

wapi ntakopa bila salary slip?

Ludger

Member
Joined
Dec 7, 2012
Posts
24
Reaction score
4
hi wana J.f.
Nimeajiriwa mahala fulani, lakini hadi sasa napokea kwa kutumia bahasha. Nimeanzisha biashara yangu kwa mwezi mmoja sasa ninahitaji mkopo kwa ajili ya kupanua biashara yangu. baada ya survey, sehemu karibu zote walihitaji biashara iliyoanzishwa miezi sita ilopita au salary slip. wanajamii naomba njia itakayonisaidia kupata milion moja na nusu.
 
kwenye saccos ya ofisini kwenu ua mtaani.

ikishindikana kwenye saccos basi jiunge na vikundi vya kibati(vipo hapo mtaani kwako) na uwaombe uwe wa kwanza kuchukua mzigo. huko ni kujuana tu hakuna mambo ya salary slip, vitambulisho wala barua ya mwajiri!
 
SACCOS na Kibati ndo mpango mzima. lakini umenishangaza mwezi mmoja tu wa biashara imeanza kuyumba?
 
SACCOS na Kibati ndo mpango mzima. lakini umenishangaza mwezi mmoja tu wa biashara imeanza kuyumba?

Thanks Class... si kwamba nimeanza kuyumba kwa mwezi mmoja, rejea post..... nataka panua biashara kwa kuwa nimeanza kwa laki tatu so demand imekuwa kubwa kiasi cha kushindwa kutoa huduma vizuri.
 
kwenye saccos ya ofisini kwenu ua mtaani.

ikishindikana kwenye saccos basi jiunge na vikundi vya kibati(vipo hapo mtaani kwako) na uwaombe uwe wa kwanza kuchukua mzigo. huko ni kujuana tu hakuna mambo ya salary slip, vitambulisho wala barua ya mwajiri!

nimekupata Zagawi, but ofisini kwetu hatuna saccoss nilikuwa mtu wa kwanza kutoa hilo wazo na sasa ndo kwanza tunataka anza mchakato.
 
Mama D.
ningefurahi kama tungefahamiana ukaniunganisha katika SACCOS unayoifahamu

Kweli tuna succos ila hii ni ya wana-ukoo tu....
Jaribu mtaani kwako huwezi kosa bhana
 
Back
Top Bottom