Ndugu yangu nilikosa deal moja kubwa sana mwaka 2015. Nakumbuka niliweka uzi hapa kuwalaumu TFF na Vilabu kwa kukosa kumbukumbu muhimu.
Nilipata deal na watu wa BBC sport ili nifanye nao kazi ya kutengeneza historia za timu ya taifa na vilabu vikongwe pamoja na wachezaji wao.
Niliyokutana nayo ni aibu.
Nilianzia TFF wakaniambia zaidi ya karatasi za usajili hakuna takwimu wala kumbukumbu zozote.
Nikatoka nikaenda Msimbazi; hapo napo sikukuta chochote zaidi ya mtu mmoja kunishauri nimwone Hans Pope. Huku napo sikupata msaada zaidi ya kupewa stori za kuifunga Zamaleck na kufika fainali ya CAF mwaka 1992 huku kukiwa hakuna hata kumbukumbu ya profile za wachezaji.
Nikaona niende Jangwani, hapo ndipo kichekesbo zaidi. Nikapokelewa kwa mbwembwe kwa kuwa nilikuwa na wazungu.
Nikauliza nahitaji historia ya Klabu na profile za wachezaji wenu. Akaitwa mzee ambaye namkumbuka kwa jina moja tu Mtoi na nikahakikishiwa huyo ndio ana kila kitu.
Nikaambiwa nimfuate nikihisi labda ananipeleka ofisini badala yake akanipekeka pale chini akaweka kiti kisha akaniambia niulize chochote kuhusu Yanga? Nikahisi kizunguzungu na kuchanganyikiwa.
Mwisho niliamua kutumia library ya UDSM upande wa magazeti na library ya Radio Tanzania Dar esalaam (Hii mnayoita TBC)
Hii ndio miamba ya soka ya Tanzania. TFF walitoa lawama kwa FAT ya Ndolanga.
Azam nao wanaelekea huko huko kwenye kutokutunza Historia ya Klabu.
Hii ndio Tanzania, hata ukiuliza Mgosi, Kichuya au Canavaro wamecheza mechi ngapi za ligi hakuna mwenye jibu.
Kila la kheri kwenye kazi yako ndugu yangu.