Wapi pazuri kuishi baada ya kustaafu?

Wapi pazuri kuishi baada ya kustaafu?

Duniani hakuna kustaafu sema ni kubadilisha majukumu tu kutokana na umri wa kisheria.Bado majukumu na wajibu viko palepale na kama hakujiandalia hazina ya miradi ya kuendesha maisha yake basi hela yake ya kinua mgongo itaisha ndani ya miaka 5 na badae ni kifo .
 
Wakuu kuna jamaa yangu anaelekea kustaafu kanitaka ushauri kuhusu sehem sahihi ya kuishi baada ya kustaafu kazi kati ya mjini na kijijini aende wapi akamalizie maisha yake ya ustaafu.

Yeye alikulia bushi ila baadae alienda kufanya maisha town kwa kitambo kirefu sana na saivi anaelekea kustaafu.
Aende kijijini akalime na kufuga ila kama ana mke sijui kama atakubali maana wana wake wingi hawakubali kuondoka mjini.
 
Wamasai wameenda kustafishwa Handeni, walipofikishwa tu wakasema tuhamie sehemu tusipochangamana na wabantu. Ndo nakubaliana kwamba pa kustafia ni vizuri ukajua ikolojia yake mapema.
 
Kustaafu siyo kufukuzwa, hivyo pa kuishi baada ya kustaafu panatakiwa kuandaliwa mapema.

Na hakuna formula kwamba wapi panafaa, kijijini ama mjini, isipokuwa ni mahali ulipojiandalia wewe mwenyewe, kiuwekezaji na kisaikolojia.

Mahali pa kuambiwa na mtu kwamba mahali fulani ni pazuri kutokana aidha na hali ya hewa ama mazingira flani ya kupendeza anavyo paona yeye bila wewe kuwa na uzoefu ama mazoea napo ni kiama.

Angalia comment # 2 katoa fact za kushiba.
...Hata wewe umetoa Facts Zilizokwenda Shule. Pongezi
 
Back
Top Bottom