Nawasalimu wale wote wapenda ukweli na uwazi
Pia napenda kuwakumbusha kila mnapopitia makala hizi basi mfanye ulinganifu na yanayotekea huko kwenye timu zenu.
Siku kadhaa niligusia namna ambavyo SIMBA imekuwa ikiulaghai umma wa mashabiki wake kwa kutumia nguvu ya mitandao, vyombo vya habari, wachambuzi na wadau wengine katika kuwalisha matangopori juu ya uwekezaji hewa uliofanyika, na ninadiriki kusema kuwa hili ni jipu kama majibu mengine.
Leo ni Machi 15, 2021 Gazeti la Championi - Jumatatu limekuja na habari kubwa kwenye ukurasa wa mbele tena kwa maandishi makubwa wakisifu namna ambavyo klabu ya Simba imepiga hatua mbele kwenye mafanikio huku wakiitupa Yanga mbali kwa mujibu wa taarifa zao za kuungaunga.
Tuelewane kuwa hakuna mwanamichezo au mpenda maendeleo aliyetayari kubeza juhudi na jitihada za kuelekea kwenye mafanikio, ila hoja inakuja namna gani maendeleo hayo yatafikiwa.
Sasa kwa pamoja tuanze kupata maelezo na kujiuliza yafuatayo[emoji779][emoji779]
Nakumbuka mara baada ya Mo kuchukua asilimia 49 za uwekezaji kwenye Klabu ya Simba imepita zaidi ya miaka miwili, sasa tuanze kwa kujiuliza tangu amechukua nafasi ya mwekezaji mkubwa kutoka kwa wanachama.
Swali la kujiuliza tangu ameichukua timu hiyo ukitoa udhamini ambao anaufanya kupitia bidhaa zake, Simba wamenufaika vipi kiuchumi?
Atakuja mtu atakuambia Simba wamefungua Mo Arena kule Bunju kitu ambacho ni upotoshaji mkubwa kwa maana uwanja wa Bunju ulikuwepo muda mrefu kabla Mo hajaingia Simba kama mwekezaji tangu enzi ya akina Aveva, Ezekiel Kamwaga ambaye aliwaamasisha wanasimba kwenda kufyeka Uwanja ulikuwepo na nyasi bandia ziliagizwa, alichofanya Mo ni kudandia gari kwa mbele na kuwafikisha standi na yeye kuwa mshindi kwa kazi ya wengine ambao leo hata majina yao hayatajwi.
Ataibuka mwingine atakuambia Simba imeingia hatua ya makundi na kucheza robo fainali katika michuano ya Klabu Bingwa chini ya Mo, ila kabla hajameza mate mwambie Simba sio mara ya kwanza kuingia makundi au kucheza robo fainali, miaka ya 1990 Simba ilicheza fainali ya Kombe la washindi; mwanzoni mwa miaka ya 2000 Simba ilitinga robo ikiwa na wakina Kaseja hivyo hakuna jipya6 ambalo Mo ameongeza zaidi ya ujanjaujanga.
Hoja ya usajili bora ambayo inasemeka ni usanii mtupu juzi tu hapa imetumia zaidi ya Sh. milioni 600 kusajili wachezaji ambao hata mazoezini hawatumiki. Halafu mtu anasema usajili bora...ni ajabu sana.[emoji2377][emoji2377]
]Ishu ya kuchukua ubingwa mara tatu hili sio geni tena hao Yanga ambao ndio wanasemwa kuwa wameachwa na Simba wametoka kuchukua ubingwa huo mara tatu huku Simba wakiteswa na hilo.
Pia takwimu zipo wazi kuwa Yanga ameifunga Simba mara nyingi zaidi, imetwa ubingwa mara nyingi zaidi sasa kusema leo Simba wanapepea ni ulimbukeni wa kiwango cha lami.
Tujiulize ile ahadi aliyoitoa Mo kuwa ataongeza idadi ya wanachama wa Simba imefikia wapi?[emoji3480]
Tuliambiwa Simba imeingia mkataba na Benki ya Equity ili kutoa kadi za uanachama sasa atoke kiongozi yeyote aseme tangu wameingia makubaliano hayo wamepata wanachama wangapi? Nina uhakika hata 10,000 hakuna.
Kusema kuwa Simba wamefanikiwa chini ya Mo ni uwongo wa wazi:
Simba hawajafanikiwa kuongeza vyanzo vya mapato wala kuboresha vile walivyo navyo.
Wameshindwa kuongeza idadi ya wanachama zaidi wameendelea kumnufaisha Mo kwenye bidhaa zake.
Wameshindwa kuweka wazi gawio wanalopata kwa mwaka kutoka kwa Mo kama faida.
Hatima ya Sh. bilioni 20 kama kifungua uchumba cha ushirika wao haijulikani.
Zimezaliwa Simba 5 ndani ya timu moja na kuweka rehani asili ya klabu husika.
Wamepoteza nembo ya asili na kuwa na simba mpya chini ya mdhamini bila wenyewe kujua.
NB Kifupi timu inapoteza uhasili wake na taratibu itakuwa mali ya familia hapo ndipo mabadiliko yatatokea kwa mujibu wa matakwa ya familia..
***** *Tukutane mtoni...