Mkuu interchange ya kibaha mbona sija isikia au ulimaanisha Ubungo
Sent using
Jamii Forums mobile app
ni overpass Mloganzila
Yajayo ujenzi wa njia sita Kimara hadi Kibaha
Madaraja mapya manne yanatarajiwa kujengwa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya njia sita unaoendelea kutekelezwa kati ya Kimara hadi Kibaha Maili Moja mkoani Pwani
BY Mwandishi Wetu, Mwananchi
mwananchipapers@mwananchi.co.tz
IN SUMMARY
Hayo yamo katika majibu yaliyotolewa kwa Mwananchi na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), kuhusu ujenzi unaoendelea unaohusisha zaidi ya kilomita 19 za barabara hiyo ambayo itakuwa ya njia sita kutoka mbili za sasa.
Dar es Salaam. Madaraja mapya manne yanatarajiwa kujengwa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya njia sita unaoendelea kutekelezwa kati ya Kimara hadi Kibaha Maili Moja mkoani Pwani.
Hayo yamo katika majibu yaliyotolewa kwa Mwananchi na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), kuhusu ujenzi unaoendelea unaohusisha zaidi ya kilomita 19 za barabara hiyo ambayo itakuwa ya njia sita kutoka mbili za sasa.
Kati ya njia hizo sita, tatu zitatumiwa na magari yanayoelekea mikoani na tatu yanayoingia Jiji la Dar es Salaam.
Majibu hayo yanatokana na maswali ya Mwananchi yaliyowasilishwa Tanroads baada ya meneja wa wakala huo Mkoa wa Dar es Salaam, Julius Ndyamukama kumwelekeza mwandishi kuwasiliana na makao makuu kupata ufafanuzi wa mradi huo.
Ofisa Uhusiano wa Tanroads, Aisha Malima alimwelekeza mwandishi kuuliza maswali kwa maandishi.
Tanroads katika majibu hayo
inasema madaraja yatajengwa Kibamba, Kiluvya na Mpiji. Pia, kutakuwa na daraja la juu (over pass) eneo la Mlonganzila.
Wakala umesema barabara ya sasa yenye njia mbili haitafumuliwa bali itaboreshwa sehemu zilizoharibika ili kuwa na ubora unaotarajiwa wa njia zote sita.
Tanroads imesema mradi utagharimu Sh140.45 bilioni, fedha zilizotolewa na Serikali.
Taarifa za awali kutoka Tanroads zilisema mradi huo ulianza kutekelezwa Agosti na unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 29, ambayo ni sawa na miaka miwili na miezi mitano.
Mradi huo unatekelezwa na kampuni ya Estim Construction Co. Ltd ya jijini Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Tanroads.
Wakala umesema wananchi waishio kando mwa Barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kibaha watarajie kupata unafuu wa usafiri kwa sababu msongamano wa magari utapungua baada ya ujenzi kukamilika.
Wakati ujenzi ukiendelea, Tanroads imewaomba wananchi wa maeneo hayo na watumiaji wengine wa barabara kuwa wavumilivu kutokana na kero ya kufungwa kwa njia za kuingia na kutoka zinazoungana na Barabara ya Morogoro.
“Tunawashauri watumie barabara za huduma (service road) zilizojengwa pembezoni mwa hifadhi ya barabara zilizopo kila upande kuingia na kutoka katika makazi yao,” inasema Tanroads.
Historia ya mradi
Takriban nyumba 2,000 zilizokuwa ndani ya eneo la mita 121.5 la hifadhi ya barabara hiyo kuanzia Kimara hadi Kiluvya zilibomolewa kupisha mradi huo kazi iliyofanyika kuanzia Julai 8, 2017 na kukamilika Desemba mwaka jana.
Baadhi ya wananchi waliobomolewa nyumba zao wanailalamikia Tanroads na Serikali kwa jumla kwa kutowalipa fidia.
Tanroads katika majibu yake imesema Barabara ya Morogoro ipo kisheria tangu mwaka 1932 na kwamba, wananchi wote waliobomolewa nyumba walikuwa wamejenga ndani ya hifadhi ya barabara hiyo, hivyo hawakustahili kulipwa fidia.
“Serikali haitawalipa fidia yoyote kwa sababu walijenga kinyume cha sheria ya barabara ya mwaka 1932, ikafanyiwa marekebisho mwaka 1967 na 2007,” inasema Tanroads.
Yajayo ujenzi wa njia sita Kimara hadi Kibaha