Wapi wanatoa kozi ya udereva wa malori kama scania, volvo n.k?

mkuu una madini kinoma,,tafadhali naomba mawasiliano yako unitumie PM nikucheki unielekeze mambo flani flani
 
Chuo kipo morogoro kihonda pale atajifunza darasani kisha ataingia barabarani akitoka hapo ameshakuwa dreva,ila itamlazimu apate mtu mwenye kusafiri nae apart uzoefu zaidi
 
Huo ni mfumo mbaya sana,mimi nilianza kuendesha bila ya kwenda huko veta na wala sikuwahi kuwa tandiboy sijui,nilikuwa najua kuendesha gari ndogo manual nikapata fuso tipper ya tani 4,nikaendesha tu,japo kuna tofauti kubwa kuendesha gari ya mzigo na gari lisilo na mzigo,

baada ya hapo nikapata scania Mende tipper,hapa ilikuwa tofauti kidogo kwenye gear shifting nilichukua manual book tu nikasoma nikaelewa nikatoa gari bandarini mpaka nyumbani,baada ya mwaka nilishakuwa mzoefu wa gari kubwa Lakini sikuwa dereva mahiri nikaingia kwenye semi trailer,hapa imenilazimu kwenda sehemu kunitumia reverse kwa muda wa mwezi,

nikasema nikaanza kufanyakazi za town trip,kutoka mizigo bandarini,kwenye ICD kupeleka kwa wateja baadae nikaanza kufanyakazi kwenye kampuni moja,nikasafiri kwenda Burundi,Rwanda,Zambia,Zimbabwe,Congo kukawa na uzoefu mkubwa sana Lakini bado sikuwa dereva mahiri,ndio nikapata kuhudhuria workshop sub scania na pia nilipokuwa nafanyakazi wakaajiri mwalimu wa madereva nikasoma mwezi mzima nikaona tofauti nilivyokuwa naendesha kabla ya workshop na baada ya workshop
 
udereva malori uzoefu ni muhimu sana , kiliendesha gari sio tabu, je aina ya uendeshaji wako uko vipi?ni salama kwako binafsi na gari lenyewe. zipo sehemu ukichezea gear gari litashindwa kwenda, ama hata kuharibu engine ,kukata shaft ,gearbox n.k. izi workshop zipo kwa usahihi sababu technolojia inakua gari za kisasa mifumo ya kisasa. ...dereva anapaswa kuifahamu mifumo hiyo. umeenda safari gari imepata itilafu ndogo tu inashindwa kwendelea na safari umngoje fundi atoke kilometa 300
 
Unajua gari ni kama mke nyumbani unakaa nae kila siku akinuna unajua leo nimemvuruga kwa namna moja au nyingine na tatizo kwenye gari uwa mara nyingi uanza taratibu mpaka kufikia kuaribika kabisaa, dereva mtaalam lazima ajue chombo chake anachokitumia, kwa sababu ufanyaji wake wa kazi inakuwa tofauti na siku zote, na siku zote gari kabla ya kuanza safari lazima ufanye ukaguzi wa nyuzi 360 kuanzia kulia kwenda kushoto juu na chini kuangalia kila kitu kipo sehemu yake, kisha kuliwasha gari ndipo kuanza safari, hii kazi hapa kwetu imekosa heshima tu lakini ni taaluma
 
Posho ya dereva kwenda lubumbashi na hilo kontena ni kiasi gani? Hiyo posho unatakiwa uitumie ndani ya muda gani?
 
Yaani hapa ndo shida ilipo mkuu gar kupatikana hiki ndicho kinatafutwa pa kuanzia maana Nit unatakiwa uwe unajua wao wanakupiga kozi fupi tu sio namna ya kuweka gia na kusepa
NiT ni kama wanakuhakiki tu na kukupa cheti hawakufundishi zaidi unapewa vikwazo tu ukivishinda unakuwa certified!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…