Huo ni mfumo mbaya sana,mimi nilianza kuendesha bila ya kwenda huko veta na wala sikuwahi kuwa tandiboy sijui,nilikuwa najua kuendesha gari ndogo manual nikapata fuso tipper ya tani 4,nikaendesha tu,japo kuna tofauti kubwa kuendesha gari ya mzigo na gari lisilo na mzigo,
baada ya hapo nikapata scania Mende tipper,hapa ilikuwa tofauti kidogo kwenye gear shifting nilichukua manual book tu nikasoma nikaelewa nikatoa gari bandarini mpaka nyumbani,baada ya mwaka nilishakuwa mzoefu wa gari kubwa Lakini sikuwa dereva mahiri nikaingia kwenye semi trailer,hapa imenilazimu kwenda sehemu kunitumia reverse kwa muda wa mwezi,
nikasema nikaanza kufanyakazi za town trip,kutoka mizigo bandarini,kwenye ICD kupeleka kwa wateja baadae nikaanza kufanyakazi kwenye kampuni moja,nikasafiri kwenda Burundi,Rwanda,Zambia,Zimbabwe,Congo kukawa na uzoefu mkubwa sana Lakini bado sikuwa dereva mahiri,ndio nikapata kuhudhuria workshop sub scania na pia nilipokuwa nafanyakazi wakaajiri mwalimu wa madereva nikasoma mwezi mzima nikaona tofauti nilivyokuwa naendesha kabla ya workshop na baada ya workshop