Pia Mitaa hiyo kama alivyosema mtanguliaji karibu na soko la kisutu na Hotel ya Chef Pride kuna duka linaitwa Tuff spares na duka lingine lipo kama unaenda kule duka la Tronics Morogoro road , linaitwa Morogoro Store pia wana vipuri vya magari ya ulaya, BMW, Benz,Audi, Range Rover na kadhalika
Kwa bei jipange zingine unaweza shangaa kama hauna uzoefu na gari za ulaya wana bei juu mno
Na kuna jingine kama unaenda Mikocheni mbele ya ofisi ya Zantel pale kabla ya kufika shoppers pia kuna duka nafikiri linaitwa Jerry spares ,
Pia Sinza/kijitonyama karibu na mabatini police station kuna viduka mbele hapo kwa mambo ya vitu vidogo vidogo kama filters na oils na mambo ya shows wanauza unaweza pata
Mie toka nijue bei za huku zipo juu nikiona hapa kama ntatoa pesa nyingi kwa baadhi ya spares nina ka channel ka Uturuki, najiagizia spares zangu nafunga na chombo ipo barabarani . Niliwahi kujichanganya nikapeleka pale Noble motors nilikoma
Shida ya gari za ulaya ni spares zake na mafundi tu kwa huku kwetu lkn mie haunitoi huko kwenye European Cars kamwe