Wapi Waziri Sonyo?

Wapi Waziri Sonyo?

kaeso

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
548
Reaction score
97
Jamani huyu mwanamuziki yupo wapi kwa sasa, jamaa alikuwa na sauti nzuri sana enzi zake akiimba sambamba na Banza Stone pale TOT Plus.
Mwenye taarifa alipo hivi sasa atujuze
1600032475499.png

---
Waziri Sonyo ni muimbaji mahiri nchini, amepata kung'ara na bendi za Chuchu Sound, TOT Plus, African Revolution Tamtam na Mviko Sound.

Mwaka 2009, Sonyo alikuwa akikabiliwa na shitaka kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tanga akidaiwa kula njama na kuiba pikipiki, lakini Oktoba mwaka 2010 alipewa adhabu ya kifungo cha nje kutokana na kukutwa na hatia ya kupatikana na pikipiki ya wizi.

WAZIRI SONYO ENZI ZAKE AKITIA MASAUTI

Kwa sasa WAZIRI SONYO yupo mkoani Tanga ambapo yupo na band ya NYUMBANI CLASSIC BAND ambao itakua ni band ya hotel huku wakisubiri ukumbi wao mkubwa wa jijin Dar-es-salaam uishe ili wahamishie majeshi jijini na kuanza upinzani na band zinazotamba na kutikingisha jiji lakini kwa mujibu wa waziri Sonyo amesema tayari wapo mbioni kuitoa album ya nyumbani clasic band ambayo itakua na nyimbo sita ikiwamo NAZIHESABU HATUA ZANGU ambao ni utunzi wake mwenyewe huku band hiyo ikiwa na mwanadada anaejulikana kwa jina la lady ambae ni mzoefu wa nyimbo za copy inagawa vile vile akitegemea kutengeneza nyimbo ambayo itaingia katika album ya NYUMBANI CLASSIC BAND

SONYO pamoja na mashabiki wake kummis toka alivyoenda jela lakini kwa sasa anaamini kuwa mwanzo mzuri wa kung'ara tena ndio huu na mashabiki wake wavute subira mengi mazuri yaja kwa waziri Sonyo na band yake ya NYUMBANI CLASSIC.
 
Duh, umenikumbusha mbali sana kwa kweli jamaa alikuwa mkali sana, nakumbuka mara ya mwisho alikuwa na bonge la soo polisi amekaa rumande kwa muda kidogo ila nasikia kesi ilikwisha na jamaa yuko dar kwa sasa, alijaribu kurudi tena kwenye mziki ila naona mambo hayajamwendea vema, natamani sana kumsikia tena huyu jamaa? bonge la mtu ila ukimsikiliza sauti utashangaa.
Nakumbuka hiki kipande alichoimba wakati yuko TOT.... kwa kuwa kuwa vimekuwa dhairi machoni pangu maji ya shingo yamenifika nashindwa kuvumilia.....................
 
Jamaa kuna kipindi alikuwa na kesi ya ujambazi, sijui ile kesi iliishaje.
 
Mara ya mwisho alikuwa Moshi mjini hii ilikuwa mwaka 2009 nilimuona na Band 1 hivii
 
Waziri sonyo kwa sasa yupo mitaa ya moshi anafanya kazi ya u-mc kwenye masherehe, mara ya mwisho tulimchukua kwenye ubatizo kula machame mronga ilikuwa december 2011.~~~
 
Kwa hiyo kwa sasa hafanyi muziki tena?
 
kuhusu waziri sonyo ngoja tummulize waziri mkuu
 
Waziri sonyo yupo tanga anafanya mziki bado ni kiongozi wa bendi flani inapiga pale nyumbani hotel tanga!anazidi kunenepeana mpaka anakuwa wa duara
 
Mbona jamaa yuko fesh tu kule Tanga! Tena jana tu nilikuwa nae...of coz kanenepa kwa vile mambo yake yako kwenye mstari.
 
Yupo Tanga kwa sasa fika nyumbani hoteli kuna live band inapiga baadhi ya siku..bado anatisha kimtindo!!
 
just about a month ago n ilikumbana naye tanga, kuna hotel mpya pale inaitwa nyumbani hotel ana bendi yake wanapiga zilipendwa, na inaonekana yuko apo kwa mda kwani it looked like amejitengenezea popularity flan, bendi inapiga vizuri i think ameamua ku settle apo!
 
mwaka jana mwishoni nilimuona kontena bar pale kibaha maili moja anafatisha nyimbo za lucky dube kwenye mic..kwa ufupi alikuwa anaganga njaa...
 
TUMY,

Niliwahi kumuona Moshi wakati fulani nilienda kwenye harusi ya rafiki yangu mmoja mchaga....
 
Back
Top Bottom