Wadau kwa bahati nimetembelea vyuo vikuu kadhaa duniani but sijawahi kuona chuo chenye kukosa utaratibu kama pale UDSM fikiria ati kumeanzishwa Stendi kadhaa za Pikipiki a.k.a Bodaboda ndani ya Chuo na wapiga debe wa daladala wanapiga kelele kama vile wapo stendi ya Ubungo . nifahamuvyo mimi Chuo kikuu ni sehemu ya kuheshimika na inahitaji utulivu wa hali ya juu maana Wahadhiri na wanafunzi wanhitaji utulivu kwa ajili ya kujifunza, kufanya utafiti na shughuli nyingine za kijamii, nikawa najiuliza Uongozi wa UDSM wameliona hili ama wanasubiri mpaka madhara yake? . Jifunzeni kwa jirani zenu (Mlimani City, Japo sio Chuo kikuu) hawaruhusu kuweka Stendi ndani, Mukandala umelala bado? au ndo unajiandaa kustaaafu baba? maana natambua unafikisha miaka 60 mwaka huu 2013 but nimjuavyo Mkulu Jei Kei atakuongezea mpaka angalau 2016 usihofu.