Pre GE2025 Wapiga kura, hakikisheni mnapiga kura kwa serikali iliyopo, viongozi mbadala hawana rasilimali za kutekeleza wanayoyaahidi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hivi hujisikii aibu, warudishe wamasai kwao, rudisheni bandari zetu, maisha yanekuwa magumu hakuna ajira, fedha yetu imeshuka thamani sana, dollar hakuna kwenye bank na bureau de change, turudishieni waliopotea au tuonyesheni makaburi yao, fedha zikizopotea (CAG) aidha zirudishwe au waliokula wafungwe. Mlifanya hayo tutawaamini nje ya hapo hata mtoto wa kambo anaweza kuwa Rais
 
Hao CCM wanatoa wapi rasilimali za kuleta maendeleo kwa wananchi?Mbona umeandika bila kutafakari?
 
hebu jaribu kufikiria,
unamchagua mtu ambae hana uwezo, hakubaliki na wananchi, hana sera wala mipango ya maendeleo ya kimkakati na kimageuzi..

analalamika tu mwanzo mwisho 🤣
Leteni maonesho ya chawa kule Arusha,ndio maana mkasema eti Magufuri mwendazake anatekeleza sera za CHADEMA,eti acheni kupinga,halafu leo jipya.
 
CCM huteseka sana kwa uchaguzi ambao sanduku la kura halisafirishwi,hapa kura zitapigwa na kumjua mshindi palepale.
 
Kuna mzee mmoja asiye na meno alikutwa akicheka hadharani na kushangilia kisa tu ameng'olewa meno na mzingu. Hakujua kama hatokaa atafune vitu vigumu.
 
Leteni maonesho ya chawa kule Arusha,ndio maana mkasema eti Magufuri mwendazake anatekeleza sera za CHADEMA,eti acheni kupinga,halafu leo jipya.
Ni muhimu zaidi kujipanga na kujiandaa vyema kwaajili ya uchaguzi muhimu wa kihistoria Nov 27,2024...

chagueni viongozi makini wenye sera za kueleweka wa CCM 🐒
 
Zinazotumika ni Kodi za wananchi,

Hivyo wananchi walipakodi wakiwepo, chama chochote kinaweza kuongoza mgawanyo wa Kodi hizo.

Wananchi Wachache chama wakitakacho wasipangiwe
 
Watakua wamekusikia ila kura ni siri.
 
Bora unge jambuli naona umekunyiro hadharani.... What a waste!!
 
Ni muhimu zaidi kujipanga na kujiandaa vyema kwaajili ya uchaguzi muhimu wa kihistoria Nov 27,2024...

chagueni viongozi makini wenye sera za kueleweka wa CCM 🐒
Mwendazake amekwenda anapostahili lakini aliwaweka wote kabisa chama kimoja na hao makini wenye sera za kueleweka na bado mtindo ni uleule shaitwan!
 
Mwendazake amekwenda anapostahili lakini aliwaweka wote kabisa chama kimoja na hao makini wenye sera za kueleweka na bado mtindo ni uleule shaitwan!
CCM imejengwa katika msingi wa umma, msingi wa wanachama wote katika umoja, akiondoka moja kwasababu zozote zile succession plans ina take place smoothly bila mbambamba yoyote..

ndiyo maana unaona huko kanda ya ziwa Rais aliko, watoto,akina mama na wazee hakuna anaetamani kubaki nyumbani. Kila moja anatamani kwenda kujumuika na Rais aliko...

Hebu check hiyo love ya kizalendo kwanza 🐒
 
Nacho jua siasa na democracia ni vitu vipo parallel .

So wewe naona unataka kutuambia vipo papendicicular.

Nukuu ya baba wa taifa.
""UTII UKIZIDI SANAA HUZAA UOGA, UOGA UKIZIDI SANA HUZAA UNAFIKI NA KUJIPENDEKEZA NA MWISHO WAKE NI MAUTI""
 
Kuna sehemu nilisoma kwamba in Africa, Watanzania ndio watu wenye IQ za chini zaidi; mwanzoni nilikua naona kama tunatukanwa; maandishi kama haya sasa hvi unaji teteaje?
 
Yale yale maupumbaf ya 1995 yameanza tena mwaka huu!

Nikadhani miaka takribani 30 kizazi cha washenzi kilishaisha, kumbe bado kipo tu!

Kila mtu anajua yeyote anayeshinda uchaguzi hukabidhiwa ofisi za umma na kwamba ofisi hizo haziendeshwi kwa rasilimali za vyama, bali kwa rasilimali za umma, hilo lipo wazi.

Guts za kudanganya danganya watu wewe umazitoa wapi!?

Maana hata kama ni chawa unatakiwa uwe 'njema' kichwani ili uweze kujenga hoja zenye mshiko, si kama hoja za namna hii za kijinga jinga, ambazo hauwezi kueleweka.
 
Usiache dozi yako uliyopewa mirembe
 
Kwa sasa Watanzania walio wengi wanao uelewa mkubwa kuhusu vyama vingi/vyama mbadala na umuhimu wake. Yale ya kuambiwa kuwa "msiwachague wataleta vita", SI KWELI na hata hili la kuambiwa "msiwachague hawana miundombinu" SI KWELI.
Kama CCM kuna maeneo wamefanya vizuri watachaguliwa tena bila shida, lakini kama kuna maeneo walizembea, watarajie pie kuangushwa!
TUWAACHE WANANCHI WAFANYE MAAMUZI BILA SHURUTI WALA HIYANA..
 
Ki vipi? Sio kwamba: sio chama chenye rasilimali, bali tunachotaka ni viongozi kutoka chama chochote rasilimali ni za nchi na kodi hutolewa na wananchi kuendesha serikali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…