Ndugu yangu ngoja pia nikukumbushe kitu. CCM wamebiresha orodha ya wanachama wao waminifu kwa mfumo mpya wa kidigitali. 2015 walikuwa na wanachama milioni8. 2020 CCM inawanachama waminifu zaidi ya milioni 14. Kwahesabu rahisi ni kwamba katika wapiga kura ambao ni zaidi ya milioni 29 wanaccm tayali wanawapiga kura milioni 14. Sasa unaweza kuona ushindi wa kimbunga utakavyopatikana kwa JPM. Ndiomana leo kama uliona mheshimiwa Jakaya mwenyekiti mstahafu alimhakikishia ushindi mkubwa JPM. Unaweza kubishana na data kama na wewe utaleta data zako full stop.
Ccm inaweza kuwa imeuza kadi hata 20m acha hiyo milioni 14. Lakini ccm haina uwezekano wa kuwa na wanachama wanaokaribia 5m wenye mapenzi ya dhati. Watu wananunua kadi za ccm kwa ajili ya kupata upendeleo wa kimfumo kama mikopo, kufanya biashara nk, na kwa kuwa kadi hiyo inauzwa chini ya shilingi 1,000 hakuna anayeona tabu kuinunua.
Mfano mrahisi, kuna jamaa zangu wanaofisi kwenye majengo ya ccm, hivyo walishawishiwa kuwa na kadi ya ccm ili kuweza kupata mkopo. Na kweli wote watano wana kadi za Ccm, lakini hawana mahaba yoyote na ccm, na kura zao wote ni cdm. Mfano huo ni mmoja ya kadi nyingi za Ccm walizouziwa watu.
Wanachofanya ccm ni kutumia idadi ya kadi walizouzia watu, na sio wanachama wa kweli kutaka kuhalalisha ushindi wa hujuma. Na ifahamike nchi hii haijawahi kutokea kiongozi anayepika data kama Magufuli, hali hiyo tunaiona kwenye data za serikali, na alikuwa na tabia hii toka alipokuwa waziri.
Nakumbuka kuna wakati alikuwa anataja idadi ya samaki na mayai yake nchini wakati akiwa waziri wa mifugo. Tabia hiyo binafsi ya Magufuli ya kupika data, ndio kaingiza serikalini na ccm respectively. Sasa hivi jaribu kufuatilia miradi ya awamu ya tano, yote utasikia iko juu ya 80%. Mfano reli SGR toka mwaka jana tunaambiwa iko 85% kipande cha Dar-Moro na tuliambiwa novemba mwaka jana itakuwa imekamilika kipande cha Dar-Moro, fuatilia ulete mrejesho.