Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mamlaka ya Uhifadhi na uendeshaji wa Mji Mkongwe Zanzibar kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali zimekubaliana kuwaruhusu vijana wa wapiga makachu katika eneo la Forodhani kuendelea na Shughuli zao kwa kuzingatia taratibu zilizoanishwa katika mikataba itakayosainiwa na vijana hao
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi Ali Said Bakari ameeleza hayo ikiwa ni takribani wiki moja kwa vijana hao kuwekewa katazo la kupiga makachu katika eneo la Forodhani baada ya kuikukwa taratibu ikiwemo suala la maadili na uharibifu wa mali za serikali katika eneo hilo
Amesema shughuli za makachu zitaendelea kwa vijana watakaokua tayari kusaini mkataba na kuridhia masharti yaliyowekwa ili kufanya shughuli hizo bila ya kuvunja sheria na taratibu za nchi
Shughuli za upigaji makachu zitaanza rasmi Desemba 31, 2024 ikiwa ni sehemu pia ya kuukaribisha Mwaka mpya wa 2025 ambapo shughuli hizo zimekua ni sehemu kubwa ya ajira kwa vijana hao ambao waliathirika na katazo hilo kwa takriban wiki moja
PIA SOMA
- Zanzibar yapiga marufuku upigaji wa makachu Forodhani hadi serikali itakapoandaa utaratibu maalum wa shughuli hiyo