Wapiga picha na walio wai kupiga picha kujeni hapa

Wapiga picha na walio wai kupiga picha kujeni hapa

VINICIOUS JR

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2022
Posts
208
Reaction score
518
Kwema ndugu zangu, leo nikiwa naelekea kuwapelekea wateja picha mtaani, nimekutana na binti mmoja akiwa na watoto wawili. Nikiwapita hadi mbele kidogo, nikashangaa kuna dogo ananifata na kuniambia, "Dada anasema uje umpige picha Jumatatu." Sasa ikabidi nigeuke, nikamwona huyo dada kasimama. Ikabidi nimuite kwa ishara, akaja akanipa maelezo kama aliyonipa dogo.

Nikamuuliza unakaa wapi, akanielekeza kuwa nyumba yao ipo pale nyuma. Nikamwambia mimi sipafahamu, basi nipe namba ya simu nikija nikuchukue. Akaniambia hana simu, tukakubaliana nitafika hiyo Jumatatu hapo alipo nielekeza. Basi bwana nikasepa, nimeenda hadi mitaa flani ya mbele kidogo huko, nimetumia lisaa lizima.

Sasa wakati narudi mishale ya saa 12, nikapita njia ileile nashangaa namkuta yule binti. Alivyoniona akatabasamu kisha akaniambia, "Nilikuwa nakusubiri nikuoneshe nyumbani." Kwanza nikaduwaa, nikajiuliza yani huyu kasimama muda wote huu kunisubiri anioneshe kwao? Je, ningebadili njia angenisubiri hadi saa ngapi?

Basi bwana akanieonesha mjengo flani ambapo ndio kwao, una bonge la fence pia wanafuga mbwa wakali. Ila sasa kaniambia anaweza kunisubiri hapo nilipomkuta, ila nisipomkuta niende humo mjengoni. Sasa hapa nawaza, hao mbwa na ndugu zake hawataniwazia tofauti endapo siamkuta hapo aliponiahidi au nisipomkuta nivunge, wakuu?
 
Wewe njoo tu nyumbani hao mbwa wala usijali hawatafuni kabisaaa, sisi haja wetu ni viungo vya mwilini mwako tu mjini hapa nyeg..e zako kipato chetu😂😂
 
Wewe njoo tu nyumbani hao mbwa wala usijali hawatafuni kabisaaa, sisi haja wetu ni viungo vya mwilini mwako tu mjini hapa nyeg..e zako kipato chetu😂😂
sasa mambo ya nyege yanatoka wap mkuu?
 
Back
Top Bottom