Gladie Sephania
New Member
- Aug 24, 2022
- 1
- 3
Yapata majira ya jioni siku ambayo bibi yangu alirejea toka kazini akiwa na malalamiko sana na akiwa mwenye kuwaza mambo mengi yanayosumbua akilini mwake pasipo kupata ufumbuzi. Ndipo niliamua kumuita bibi yangu nakuanza kumuuliza kitu gani hasa kinamsibu 'Bibi shikamo, pole na mihangaiko ya shughuli' bila kupoteza muda bibi aliitikia salamu hiyo na kuanza kuniambia kuwa mjukuu wangu "Wapiganapo tembo nyasi huumia" kimya kidogo kilitawala, ndipo alipoanza tena kueleza kuwa miaka ya nyuma watu wengi walikuwa wakitumia njia za asili zaidi katika ufanyaji wa shughuli zao na zilifanyika kwa ufanisi mkubwa mno, hakuishia hapo alianza sema wengi tulikuwa tukitumia vibubu, viboksi na hata vichupa vidogo sana vilivyo na kisehemu/mpenyo mdogo tu uliomwezesha mtu kuhifadhi pesa, walifanya hivo kwa mara zote bila kuwa na hasara wala punguzo lolote lile.
Hodii!, Kabla hata ya bibi kumaliza kuelezea historia hiyo ilisikika sauti upande wa pili ikibisha hodi. Baada ya kuchungulia nje ndipo tulipogundua kuwa ni Kigogo mmoja aliyekuwa akiaminiwa na kukubaliwa na kila mmoja mtaani pale amekuja nyumbani baada ya kukaa miaka miwili ughaibuni. Ndipo bibi alipoamuru iandaliwe kahawa kwajili ya huyo mgeni wakiwa wanaendelea kubadilishana mawazo na kuendelea kujadili gharama za maisha ya karne ya 21. Maisha yamekuwa kasi mno na kila uchwao vitu vinakuwa na gharama kubwa alisikika akiongea huyo bibi yangu.
Ndipo nami nikapata wasaa wakumuuliza kigogo huyo kama kuna uhusiano wowote kati ya ongezeko la bei ya vitu na gharama zinginezo na vita vinavyoendelea katika nchi zingine. Ndipo yule Kigogo alitikisa kichwa chake kwa kutaka kukubaliana na hilo na akaendelea kuelezea kuwa hivi vyote vinatokana na nchi kuwa tegemezi zaidi wa hivyo vitu ndio kunasababisha uhaba na ongezo la gharama hizo kwa kiasi kikubwa, “Unahitaji moyo wa bati na jicho kama la mwewe ili uweze kuona na kutafakari mafanikio ya kila mmoja wetu bila kujali hali yake aliyonayo kwa muda ule maana urefu wetu wa mikono unatofautiana, hakuishia hapo aliendelea kusema” Jengeni kwa fito kama matofali yakivunjika vipande wanangu…….... nawasihi, baada ya kuona mimi na bibi yangu tukimsikiliza kwa makini na hadhari kubwa.
Palitawala nyuso za kufikiria na kuwaza lakini majibu yasipatikane ndipo Kigogo huyu aliponigeukia na kuniita mjukuu wa bibi tega sikio lako vizuri, ndipo alipoanza sema maisha ya Dunia ni milima na mabonde usipopanda basi utashuka, pigania kile ulichonacho na vinginevyo, usipoteze wakati na kuenenda na nyakati ndio silaha kuu. Kuenenda na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yatakuza zaidi uelewa wako na pia kuwa na elimu zaidi kuhusu mseto, heshimu kila mtu, jali vya watu na pia sikiliza kila mmoja lakini utendaji wako uendane na vile matakwa yako yanavoridhia na kuona nini hasa unatakiwa kufanya. Lakini baada ya maongezi yote hayo aliyoniambia nikawa bado na kiza kinene akilini mwangu kuhusu neno mseto ndipo nilipomwuliza kwa ufafanuzi zaidi nakuniambia lazima kuwepo na mgawanyo wa majukumu kwa ajili ya ufanisi na uzalishaji zaidi kuliko kutegemea chanzo kimoja.
Masaa yalizidi kusonga mbele ndipo alipoamua kuondoka na kumwambia bibi kuwa anarudi ughaibuni ila tuendelee kuyafanyia kazi na kuyatii yale yanayotupasa na panapo majaliwa atarudi tusalimu akirudi huku kwetu.
Chanzo: Raging bull elephants fight for supremacy (and the girls) in ferocious clash on plains of Africa

Upvote
3