Wapigania Uhuru waliwapotosha Waafrika

Wapigania Uhuru waliwapotosha Waafrika

Showmax

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2022
Posts
6,592
Reaction score
12,707
Wapigania UHURU waliwadanganya waafrika wawasapoti kuwafurusha wakoloni baada ya wakoloni kuondoka watawala wakageuka kuwa madikteta wakawageukia waafrika wakaanza kuwatesa waafrika.

Unapigania UHURU kuwaondoa Wazungu kisha unaunda makundi ya kigaidi, wasiojulikana na kihalifu (vikosi vya kumlinda Rais) vikulinde dhidi ya wanaotaka kukuondoa kisa utendi haki, kwa kwenda kinyume na matarajio ya wananchi, kwa kuviamuru vikosi vyao vya kigaidi kuteka, kutesa na kuua watu kwa mtindo wasiojulikana Ili kulinda tumbo.

Sasa nini tofauti yako na wakoloni, angalau wakoloni walifanya hayo huku wakiletea watu maendeleo. Thus huwa nasema wapigania UHURU walipigania maslai yao binafsi kwa kuwatumia Waafrika na siyo kupigania maslai ya Waafrika wote; ilikuwa ni kiini macho tu.

Thus baada ya UHURU wao ndio walionufaisha matumbo yao hadi SAsa vizazi vyao huku mamilioni ya waafrika wakitopea kwenye lindi la ufukara. Ukifanya study utagundua angalau mwafrika alikuwa ana nafuu kabla ya UHURU ajira zilikuwapo tele, chakula tele, elimu na afya zilikuwapo tele.

Walipigania UHURU ndio walipotosha waafrika walikuwa na ajenda binafsi za maslai yao wao thus baada ya UHURU wakageuka kuwa wakoloni weusi kwa kuwatendea mabaya waafrika, huku wakipora fedha na kuzificha ulaya.

Wakatumia elimu zao kuzibomoa nchi zao (Mugabe, Kamuzu banda, Savimbi, nk), wakajimilikisha utajiri wa nchi wao binafsi na familia zao ( Moi, Kenyatta, Mobutu, Do santos, nk) hawana historia ya kumiliki mali kabla ya uongozi zaidi ya kuwapora wananchi kupitia madaraka.

Asilimia 90 ya waafrika ni dhoofu hali, angalau kidogo nchi za waarabu zilizopo Afrika na hizi zimesaidiwa na mfumo wa dini ya kiislamu unaowafundisha watawala kutenda haki.

Ukuwahi kusikia gavana au mtawala yeyeto wa kikoloni amewahi fisadi mali ya nchi kwa maslai binafsi kama alivyofanya Zuma, Mobutu, nk kupendelea kwao. Mugabe kujenga makasri ulaya na singapore hali yeye ni mtawala wa kiafrica.

Unafukuza wakoloni kwamba unaweza then unawahitaji tena kwa lugha ya kuwapamba ukiwaita eti wawekezaji, nini SAsa tofauti ya mkoloni na Mwekezaji, angalau mkoloni hakuwaza kuondoka thus alijenga miundombinu mbalimbali nchini iliyo hai hata sasa.

Wakoloni hawakutegemea kodi kuleta maendeleo nchi za Afrika bali walitumia raslimali tele zilizojaa mfano nguvu kazi, madini, maji, ardhi, misitu nk, leo watawala wa kiafrica wameshindwa japo Wana KILA kitu yaani pesa, ardhi, maji, watu, masoko, nk, hawana tofauti na mabus ya mwendokasi wamepewa KILA kitu kuanzia abiria, barabara, magari lakini bado hawawezi.

Naona kama waafrika tumegota kujitawala. Ni rahisi kwa mtawala wa kiafrica kuiba pesa za wananchi akaenda kununua mabus, malori au kudhamini timu ya mpira au kuficha pesa Ulaya. Huku akimuacha mwafrika mwenzake anakufa kwa kukosa panadol, maji, njaa, nk.

Niseme tu watawala wa kiafrica walipigania maslai yao binafsi kwa kuwahadaa waafrika kwa malengo yao binafsi na sio malengo ya jumla, thus ukigusa maslai yao lazima wakuweke kwenye kiroba.
 
Hata somo la historia mashuleni tulipotoshwa zaidi ya kujengewa tu chuki Ili kuhalalisha kushindwa kwa watawala kutuletea maendeleo.

Thus wakawatumia waandishi kama kina Walter Rodney kusema uongo kueneza propaganda za chuki Ili kuwapumbaza waafrika wajue matatizo yao yametokana na kutawaliwa.

Huu ni uongo mkubwa kabisa, kutawaliwa Katu hakuifanyi nchi kuwa masikini, USA, China, India, UK zilitawaliwa lakini baada ya UHURU zilianza upya kwa kuyatumia maarifa zikawa juu.

Vipi nchi za kiafrika ambazo hazikutawaliwa mfano liberia, ethiopia mbona nazo ni masikini SAwa na nchi zingine za kiafrica. Nchi za kiafrika karibu zote maisha ufanana.
 
Kama Nyerere, mkoloni aliruhusu kuundwa kwa vyama vya siasa na vyama vya wafanyakazi vyenye nguvu, Ila Nyerere alidai uhuru kisha akafuta vyama vyote vya siasa ambavyo mkoloni alikuwa karuhusu, na kugeuza vyama vya wafanyakazi matawi ya CCM (TANU kipindi hicho)

Nyerere alikuwa mzuri kwenye siasa na sio kwenye uchumi.
Aliua uchumi alioachiwa na wakoloni.
Kambona alikuwa sahihi
 
tulitapeliwa kwaio!.
kuanzia miaka 60's ya vuguvugu la uhuru nchi za Africa mpaka sasa ni watu wachache wenye kuzunguka cicle za watawala ndo wanafaidi matunda ya uhuru.

We uoni walituingiza chaka, ajira hakuna, kilimo akilipi, vijana wapo bize wanazurura embassy za Ulaya wakabebe box, wengine wanakufa maji wakizamia ulaya kufuata maisha.
Shida ni uongozi na sio mazingira
 
We uoni walituingiza chaka, ajira hakuna, kilimo akilipi, vijana wapo bize wanazurura embassy za Ulaya wakabebe box, wengine wanakufa maji wakizamia ulaya kufuata maisha.
Shida ni uongozi na sio mazingira
dah,noma sana.alafu wanakwambia vijana tujiajiri huku wao wakipeana madaraka na familia zao,wapo radhi kuuwa ili wabaki kua watawala.
 
Nyerere alikuwa mzuri kwenye siasa na sio kwenye uchumi.
Aliua uchumi alioachiwa na wakoloni.
Kambona alikuwa sahihi

Siasa gani alikua mzuri? kuwa Dictator au? Alifuta vyuma pinzani ni kuvipiga marufuku, Alifuta taasisi za dini pamoja na vyama vya wafanyakazi na kugeuza matawi ya Tanu.
Jamaa alikua ni Dictator mbaya sana. Tofauti yake ni Jiwe ni wakati tu zama hazikufanana.
 
Welldone mkuu,mada nyingine yenye kufikirisha,tatizo hivi vyama vinavyojiita vimeleta hii so called uhuru vimeshindwa kabisa kujipambanua kutoka freedoms fighters na kuwa vyama vya kutawala na kuongoza nchi, Tanzania sasa tuna royal families as if uongozi ni wao tu, wametumia vyombo vya dola kujijingea hii steel circle kuwazunguka,wame lose touch na masses on the ground, unamsikia minister hajui bei ya mchele hapo mbeya (unakozalishwa kwa wingi)bei inazidi 3k per kilo!,but taratibu vitafutika tu kwenye historia ya dunia,KANU UNIP, vimefutika, swapo, anc,zanu pf, frelimo vinaanza kupata ile stage 2 ya cancer, vingine vipo stage 3,ikifika 4 vinakufa!,ANC next year general election Kuna uwezekano kikaenda under 50%,kitalazimika kuingia kwenye coalitions, ccm ina fly na mtaji wa ujinga wa middle class for now
 
Waafrica mmeanza funguka akili make viongozi wenu wamefeli vibaya sana afu lawama mnampelekea mzungu
 
Hawa madikiteta wa Africa ni utopolo hasa, kisa cha Kazungula border bridge kuwa na bend ni kwa sababu Dictator Mugabe hakutaka hili daraja liingie upande wake wa Zimbabwe!!!,Leo Zimbabwe inanufaika na daraja hili kwa kupitishia mizigo yake hapo!,na elewa kukataa kwake kulileta uchelewesho wa ujenzi na gharama kuwa kubwa, hili daraja lingekua straight, pale ilipokua mpaka wa Botswana na zambia wa zamani
 
Kitu Cha kusikitisha hata sisi tunaokoment wengi wetu tukipewa uongozi tunafanya kama wanavyofanya hao tunaowasema.

Tangu tumepata uhuru zaidi ya miaka 60 imepita viongozi wengi wamebadilika lkn utendaji ni uleule.

Wazazi, ndugu na jamaa wanafurahia watoto wao wakilihujumu taifa, unakuta mzazi anajua kabisa mwanae ni afisa Tra na scale ya mshahara inajulikana lkn anapomuona analimbikiza mali hamuulizi bali atakaa maskani ajisifu mwanae yupo tra lkn mzazi huyohuyo anaanza kuponda viongozi wa serikali
 
Siasa gani alikua mzuri? kuwa Dictator au? Alifuta vyuma pinzani ni kuvipiga marufuku, Alifuta taasisi za dini pamoja na vyama vya wafanyakazi na kugeuza matawi ya Tanu.
Jamaa alikua ni Dictator mbaya sana. Tofauti yake ni Jiwe ni wakati tu zama hazikufanana.
Angalau aliwaunganisha watu Ili aweze kuwatawala kiustaraabu
 
Back
Top Bottom