- Thread starter
-
- #21
Kitu Cha kusikitisha hata sisi tunaokoment wengi wetu tukipewa uongozi tunafanya kama wanavyofanya hao tunaowasema.
Tangu tumepata uhuru zaidi ya miaka 60 imepita viongozi wengi wamebadilika lkn utendaji ni uleule.
Wazazi, ndugu na jamaa wanafurahia watoto wao wakilihujumu taifa, unakuta mzazi anajua kabisa mwanae ni afisa Tra na scale ya mshahara inajulikana lkn anapomuona analimbikiza mali hamuulizi bali atakaa maskani ajisifu mwanae yupo tra lkn mzazi huyohuyo anaanza kuponda viongozi wa serikali
Hili ni tatizo kubwa Sana mwizi kuonekana shujaa.
Hii imetokana na wazazi waliofanya Kazi KWA uaminifu na uadilifu na uzalendo Mkubwa Sana serikali ikawatupa jongoo, wakiishi maisha ya mbwa baada ya kustaafu, kumbuka Nyerere hakutaka watu wamiliki mali. Chupa za bia pembeni jamaa anakusanya vizibo kesho unafatiliwa pesa za kunywa umetoa wapi. Uhujumu uchumi unakuhusu, so ikabidi wengi wawe wazinzi wakatumia pesa zao kuhonga, maana ukifanya maendeleo tu unapewa kesi ya uhujumu uchumi. Baada ya wazee kutupwa jongoo, wakiishi KWA dhiki ndio wamewaambia vijana wao wakombe kabisa Ili kesho wasiishi maisha mabovu kama wao, thus vijana wapo radhi kugawana na hakimu Ili kumaliza soo. Pangekuwepo na utaratibu wa kuwajali wastaafu angalau vijana wasingekuwa wezi. Maana madhara ya wezi wote uathirika wakiwemo na wezi wenyewe, maana hizo pesa Sana Sana watakula watoto wao kuanzia wajukuu kuendelea ni msoto tu.
Unapoiba pesa za uma means umeiba kesho ya mjukuu wako.